Betty Sande mwanamke aliyeyabadili maisha yake kutoka katika ukahaba Kenya

Maelezo ya video, Betty Sande mwanamke aliyeyabadili maisha yake kutoka katika ukahaba Kenya

Betty Sande alikuwa kahaba kwa miaka mingi hadi alipogundua kwamba ana virusi vya ukimwi.

Mama huyo wa watoto watatu amefanikiwa kukabiliana na unyanyapaa dhidi yake kutoka kwa familia yake binafsi na hata jamii. Ameyabadili maisha yake na sasa anajihusisha katika miradi midogo midogo kujikimu kimaisha. Amemueleza mpiga picha wetu Judith wambare alichokipitia katika maisha yake ya nyuma ya ukahaba, na namna alivyofanikiwa kuyabadili maisha yake