An-Nisaa: Huduma mpya ya teksi kwa wanawake pekee Kenya
Katika miaka michache iliyopita, huduma kadhaa zimeanzishwa kupitia programu tumishi Nairobi za usafiri katika mji mkuu huo wa Kenya. Programu hizi huwahudumia kila mtu , wanaume kwa wanawake. Sasa kumevumbuliwa programu maalum ya wanawake kwa ajili ya kuwahudumia wanawake. An-Nisa imezinduliwa na hutoa hudumu kwa wanawake pekee. Madereva wake pia ni wanawake watupu. Imepokewa vizuri na wanawake wanaosema hawapendelei kusafirishwana wanaume, kutokana na sababu kama vile kidini au kiusalama.
Mpiga picha: Hassan Lali
