Teknolojia inavyosaidia kukabiliana na uhaba wa chakula Nigeria
Oscar Eponimo amevumbua programu ya kukabiliana na uharibifu wa chakula kwa lengo la kutatua tatizo la njaa. Eponimo alipata msukumo kutokana na maisha ya utoto wake yaliokabiliwa na njaa. Babake alipokuwa mgonjwa na kushindwa kufanya kazi, familia yote ilibaki kuwa na njaa. Programu yake ya chowberry inawaunganisha watu na chakula katika maduka ya jumla ambacho kawaida hutupwa katika jaa. Tayari teknolojia hiyo imechukuliwa na wauzaji 35, masharika yasiokuwa ya kiserikali pamoja na mashirika mengine nchini humo.
