Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwa Picha: Mazishi ya dada yake rais wa Tanzania John Magufuli yalivyokuwa Chato, Geita, Raila Odinga ahudhuria
Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Kenya, Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga aliungana na viongozi wastaafu wa Tanzania katika mazishi ya dadake Rais wa Tanzania Joseph Magufuli, Monica Magufuli.
Mazishi hayo yalifanyika katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.
Bi Monica alifariki dunia asubuhi ya tarehe 19 Agosti, 2018 katika hospitali ya Bugando Jijini Mwanza alikokuwa akipokea matibabu.
Rais Magufuli alikuwa amemtembea hospitalini Magufuli Jumamosi akiwa amelazwa katika Chumba cha uangalizi Maalum ICU.
Rais Magufuli akiwa anazungumza jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi mara baada ya kumaliza mazishi.
Rais Magufuli akiweka shada la maua katika kaburi la dada yake baada ya mazishi.
Rais Magufuli akiwa na Mama yake mzazi Suzana Magufuli wakati wakitoa heshma za mwisho katika jeneza.
Magufuli akiweka udongo ndani ya kaburi.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akitoa heshma za Mwisho katika jeneza.
Baba Askofu mkuu Mwandamizi Yuda Thaddeus Ruwaichi akiongoza Misa ya kumuombea Marehemu Monica Magufuli Chato mkoani Geita.
Picha zote: Ikulu, Tanzania