Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Rais wa Tanzania afiwa na dada yake
Dada yake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Monica Joseph Magufuli amefariki dunia leo tarehe 19 Agosti, 2018 katika hospitali ya Bugando Jijini Mwanza.
Hapo jana Rais Magufuli alienda kumtembelea dada yake akiwa amelazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) katika hospital hiyo ya Bugando na rais alisema kwamba hali ya dada yake sio nzuri.
Bi.Monica Magufuli alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya moyo.
Monica Joseph Magufuli amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 63 (alizaliwa tarehe 25 Novemba, 1955) na ameacha watoto 9 na wajukuu 25.