Ni miaka 20 tangu mashambulizi yatokee kwenye balozi za Marekani Dar es Salaam na Nairobi

Balozi wa Marekani nchini Kenya Robert Godec (kushoto)
Maelezo ya picha, Balozi wa Marekani nchini Kenya Robert Godec (kushoto)

Watu nchini Kenya na Tanzania wanaadhimisha miaka 20 tangu yatokee mashambalizi kwenye balozi za Marekani mijini Nairobi na Dar es Salaam yaliyofaywa na kundi la al-Qaeda,

Zaidi ya watu 200 wakiwemo raia 12 wa Marekani waliuwa kwenye milipuko hiyo ya mwaka 1998.

Zaidi ya watu 200 wakiwemo raia 12 wa Marekani waliuwa kwenye miliuko hiyo ya mwaka 1998.
Maelezo ya picha, Zaidi ya watu 200 wakiwemo raia 12 wa Marekani waliuwa kwenye miliuko hiyo ya mwaka 1998.

Mashambulizi hayo yalikuwa ndiyo ya kwanza makuu yaliyofanywa na al-Qaeda dhidi ya Marekani ndipo FBI ikamweka kiongozi wake Osama Bin Laden kuwa mtu aliyetafutwa zaidi duniani.

Al-Qaeda tena wakaishambulia Marekani miaka mitatu baadaye wakitumia ndege mbili zilizokuwa zimetekwa nyara na kuzigongesha kwenye majengo ya World Trade Centre mjini New York mwaka 2001.

Zaidi ya watu 3000 waliuwa kwenye mashambulizi hayo.

Jengo uliokuwa ubalozi wa Marekani mjini Nairobi
Maelezo ya picha, Jengo uliokuwa ubalozi wa Marekani mjini Nairobi