Selfie za watu wenye ndevu zinazoogofya

Muda wa kusoma: Dakika 2

Watu wenye ndevu wamekuwa wakijipiga aina ya selfie kutoka chini na wamekuwa wakiwaogopesha watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Baadhi ya watumiaji wa Twitter waliwaambia wenye ndevu hao kuwacha kuangalia juu kwa sababu picha hizo zilikuwa zinatisha.

Picha hizo zilianza kusambazwa baada ya mtumiaji mmoja wa twitter kutuma ujumbe akisema wanaume wenye ndevu wanapoangalia juu tazama.

Watu walijiunga na wengine kuchora nyuso za watu ili kuongezea.

Dan alituma picha zake za ndevu alizopiga picha.

Ilijibiwa mara kumi ya maelfu. Kieron alikuwa wa kwanza kujiunga.

Nikiwa ripota wa kipindi cha Newsbeat mwenye ndevu nyingi pia nilijipata nimepiga picha

Huku picha hizo zikisambazwa haraka na kwa wetu wengi kwa mufda mfupi kama ilivyo ada katika mtandao wa twitter, watu walianza kumwambia mtu wa kwanza kupiga picha hiyo kuongeza mapambo katika picha hiyo

Scott alituma ujumbe wa twitter akimtaka Dan kuchora uso katika shingo zao na wengine wakakubliano kwamba huo ndio mwelekeo.

Baadhi ya watu waliongezea macho na emoji na mtu mmoja akachora uso wake na kalamu.

Sio kila mtu alifurahia picha hizo zilizosambazwa , kuna wengine wanahoji ni nini haswa kinachowavutia katika picha hizo.