Wapalestina wengine wawili wauawa Gaza

palestinians nakba
Maelezo ya picha, Kijana akiwa ameshika ufunguo wa bandia wakati wa vurugu baina ya Waisrael na Wapalestina

.

Inaarifiwa kuwa Wapalestina wawili zaidi wamepigwa risasi na kufa katika ukanda wa Gaza wakati mkutano wa Umoja wa Mataifa ukiendelea.

Akizungumzia na mkusanyiko wa mabalozi wa Umoja wa Mataifa, Nikki Haley, ameisifu Israeli na kusema hakuna nchi itakayoweza kufanya zuio zaidi ya ilivyo.

Alisema kuwa kundi la wapiganaji wa Palestina Hamas lilikuwa likihamasisha vurugu kwa miaka mingi.

Viongozi wa Palestina pamoja na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, walizungumza walipokuwa ziarani mjini London wameliita tukio la Jumatatu wiki hii kuwa ni mauaji ya kimbari.

Njia iliyotumiwa na Israeli ya kutumia risasi za moto dhidi ya waandamanaji imelaumiwa duniani kote.