Afrika wiki hii kwa picha: 2-8 Machi, 2018

Mkusanyiko wa picha nzuri zaidi kutoka Afrika na kuhusu Waafrika maeneo mbalimbali duniani wiki hii.

Skauti wa Kike wa Kenya ni miongoni mwa mamilioni ya watu waliosheherekea siku ya Wanawake duniani siku ya Alhamisi

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Skauti wa Kike wa Kenya ni miongoni mwa mamilioni ya watu waliosheherekea siku ya Wanawake duniani siku ya Alhamisi
Mashabiki wa Gor Mahia ya Kenya wakienda nyumbani kwa mbwembwe kuiona timu ya Tunisia club Esperance katika Michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika walitoka sare ya 0-0

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Mashabiki wa Gor Mahia ya Kenya wakienda nyumbani kwa mbwembwe kuiona timu ya Tunisia club Esperance katika Michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika walitoka sare ya 0-0
Huyu ni shabiki wa Al Ahly ya Misri akiwa amewasha moto kwenye uwanja wa kimataifa wa Cairo timu yake ilishinda 4-0 dhidi ya Mounana Gabon.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Huyu ni shabiki wa Al Ahly ya Misri akiwa amewasha moto kwenye uwanja wa kimataifa wa Cairo timu yake ilishinda 4-0 dhidi ya Mounana Gabon.
Mechi hii ilichezwa kwenye kituo cha kutunza wahamiaji nchini Libya.Ilikutanisha Timu ya Senegal(Kijani) na Cameroon(rangi ya chungwa).

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mechi hii ilichezwa kwenye kituo cha kutunza wahamiaji nchini Libya.Ilikutanisha Timu ya Senegal(Kijani) na Cameroon(rangi ya chungwa).
Wacheza mieleka wa Dambe wa Kaskazini mwa Nigeria wakipimana nguvu kusini mwa Lagos. Dambe ni aina ya mchezo wa kupigana.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Wacheza mieleka wa Dambe wa Kaskazini mwa Nigeria wakipimana nguvu kusini mwa Lagos. Dambe ni aina ya mchezo wa kupigana.
Mwanakikundi wa sanaa ya sarakasi wa Kibera nchini Kenya, akipumua huku akitoa moto mdomoni wakati wa maonyesho jijini Nairobi Jumatano.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mwanakikundi wa sanaa ya sarakasi wa Kibera nchini Kenya, akipumua kwa huku akitoa moto mdomoni wakati wa maonyesho jijini Nairobi Jumatano.
Muigizaji wa Kenya Lupita Nyong'o alitumia uzi wa dhahabu kupamba nywele zake kwa mtindo kutoka Rwanda wakati wa sherehe za Oscar siku ya Jumapili.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Muigizaji wa Kenya Lupita Nyong'o alitumia uzi wa dhahabu kupamba nywele zake kwa mtindo kutoka Rwanda wakati wa sherehe za Oscar siku ya Jumapili.
Hali ya hewa ya baridi iliyokumba Ulaya Mashariki wiki hii pia kulikuwa na hali ya kuanguka kwa barafu katika milima ya Atlas nchini Morocco

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Hali ya hewa ya baridi iliyokumba Ulaya Mashariki wiki hii pia kulikuwa na hali ya kuanguka kwa barafu katika milima ya Atlas nchini Morocco
Familia hii ni moja kati ya maelfu ya Watu waliokimbia machafuko Mashariki mwa Congo.Wametumia boti kuvuka Ziwa Albert kuelekea Uganda

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Familia hii ni moja kati ya maelfu ya watu waliokimbia machafuko Mashariki mwa Congo.Wametumia boti kuvuka Ziwa Albert kuelekea Uganda
Siku ya Jumatatu, Wanaume na wanawake walionekana wakitafuta dhahabu mjini Makeni, Sierra Leone

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Siku ya Jumatatu, wanaume na wanawake walionekana wakitafuta dhahabu mjini Makeni, Sierra Leone
Uchaguzi wa siku ya Jumatano ulikuwa wa amani, isipokuwa isipokuwa maandamano yalishuhudiwa nje ya Jengo la Ofisi ya wapinzani la Sierra Leone Peoples Party (SLPP)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Uchaguzi wa siku ya Jumatano ulikuwa wa amani, isipokuwa maandamano yalishuhudiwa nje ya Jengo la Ofisi ya wapinzani la Sierra Leone Peoples Party (SLPP)
Nchini Ivory Coast, kulikuwa na maandamano yanayodaiwa kupinga vitendo vinavyoelezwa visivyo haki vya watoa huduma za mazishi.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Nchini Ivory Coast, kulikuwa na maandamano yanayodaiwa kupinga vitendo vinavyoelezwa visivyo haki vya watoa huduma za mazishi.
Kikundi cha wahamiaji wa Eritrea nchini Israel wakiwa wanapata picha ya pamoja kwa kuwa wanaondoka kwenye Kituo cha Holot nchini Israel, Kituo hicho kilicho katikati mwa Jangwa kinatarajiwa kufungwa lakini kwa sasa ni kituo huria ambapo wanaoshikiliwa wanakuwa huru kuondoka saa za mchana na kurejea usiku.Shirika la habari la Ulaya limeripoti.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Kikundi cha wahamiaji wa Eritrea nchini Israel wakiwa wanapata picha ya pamoja kwa kuwa wanaondoka kwenye Kituo cha Holot nchini Israel, Kituo hicho kilicho katikati mwa Jangwa kinatarajiwa kufungwa lakini kwa sasa ni kituo huria ambapo wanaoshikiliwa wanakuwa huru kuondoka saa za mchana na kurejea usiku.Shirika la habari la Ulaya limeripoti.