Mashambulio ya Boko Haram kwa takwimu

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amesema mara kwa mara kuwa wapiganaji jihadi wa Boko Haram wameshinda lakini uchambuzi wa BBC wa mashambulio yao unaonyesha tofuati ndogo.

Takwimu zilizokusanywa na BBC Monitoring zinaonyesha kuwa kundi hilo limewaua zaidi ya watu 900 mwaka 2017, ikiwa ni idadi kubwa sana ikilinganishwa na mwaka 2016.

Liliendeela kutekeleza mashambulio kila mwaka, na kukiuka sisitizo la rais Buhari kwamba wanamgambo hao wametimuliwa.

Tumezikusanya takwimu kuonyesha aina ya mashambulio, maeneo wanayolenga na miezi gani ndio hushuhudiwa mashambulio zaidi ya kundi hilo la Boko Haram.

Boko Haram ni nani?

Boko Haram ilianza kutekeleza mashambulio dhidi ya serikali ya Nigeria mnamo 2009 kwa lengo la kuidhinisha eneo linalolitawala kwa misingi ya kiislamu magharibi mwa Afrika.

Ukiwa umelenga kaskazini mashariki mwa Nigeria, mzozo huo unaarifiwa kusababisha vifo vya watu 20,000 na kusababisha wengine takriban milioni mbili kuishia bila ya makaazi.

Wakiongozwa na Abubakar Shekau, Boko Haram lilikiri kushirikiana na kundi la wanamgambo wa Islamic State (IS) mnamo Machi 2015.

Mnamo Agosti 2016, kundi hilo liligawanyika katika makundi kadhaa madogo baada ya IS kutangaza kuwa Shekau ameondoshwa kama kiongozi.

Mashambulio yaongezeka, maeneo yanasalia yale yale

Inaarifiwa kuwa Boko Haram lilitekeleza jumla ya mashambulio 150 mnamo 2017, ikiwa ni idadi ya juu ya mashambulio 127 linaloarifiwa kutekeleza mwaka uliotangulia.

Kaika miaka yote kundi hilo lilitekeleza kiwango cha juu cha idadi ya mashambulio yake Januari, huku maongezeko yote mawili yakifuatwa na tuhuma za rais Buhari kuwa Boko Haram limesambaratishwa.

Maeneo ambako kundi hilo imeyashambulia ni yale yale katika miaka miwili iliyopita.

Nigeria imekabiliwa na baadhi ya mashambulio hayo mwaka 2016 na 2017, huku jimbo la Borno -ulikoanzia uasi huo - likilengwa pakubwa.

Boko Haram limedhihirisha kwamba linaweza kuendelea kushambulia maeneo zaidi mwaka jana, huku kukiripotiwa mashambulio katika eneo la kaskazini Cameroon, eneo la Diffa nchini Niger na Lac nchini CHad, maeneo yote yakiwa yanapakana na Nigeria.

Haya pakubwa yanaonyesha maeneo ambayo kundi hilo iliamua kuyalenga mnamo 2016, lakini kuna tofuati ndogo kati ya miaka hiyo miwili, huku Nigeria ikishuhudia mashambulio zaidi mwaka jana huku Niger mashambulio hayo yakipungua.

Mbinu za mashambulio

Inaripotiwa kuwa Boko Haram lilitekeleza mashambulio 90 ya kujihami na mashambulio 59 ya kujitoa muhanga mnamo 2017.

Nigeria ndio ilioathirika pakubwa na mashambulio hayo, huku mbinu kuu ikiwa ni mashambulio ya kujihami.

Katika upande wa pili wa mpaka na Cameroon kundi hilo linaonekana kutumia mbinu tofuati, likitumia mashambulio ya kujitoa muhanga zaidi.

Mbinu hizo katika nchi hizi mbili zilidhihirika pia mnamo 2016.

Takwimu zinaonyesha kuongezeka kuonekana kutumika mbinu za mashambulio ya kujitoa muhanga.

Nchini Nigeria, kundi hilo liliongeza idadi ya mashambulio kutoka 19 mnamo 2016 hadi 38 mwaka 2017, na ongezeko hilo likishuhudiwa pia nchini Cameroon.

Mashambulio ya kujitoa ndio mbinu iliotumika sana katika mji wa Maiduguri NIgeria, unaoendelea kuwa kitovu cha uasi, wakati mashambulio ya kujihami yakishuhudiwa zaidi kwingine.