Jeshi laonya kutumia nguvu nyingi kuzima maandamano Iran

crowds carrying flags

Chanzo cha picha, IRINN

Maelezo ya picha, State TV showed crowds carrying flags

Wanajeshi wa Iran, wamewatisha wandamanaji wanaopinga serikali, kwamba jeshi litatumia nguvu nyingi, iwapo fujo za kisiasa zitaendelea.

Ilani hiyo imetolewa baada ya usiku mwengine wa maandamno mjini Tehran na kwengineko.

Katika sehemu fulani, pamoja na mji mkuu, majengo ya serikali yalishambuliwa.

Iranian students protest at Tehran University

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Wanafunzi walihusika katika maandamano

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Abdolreza Rahmani-Fazli, aliwatuhumu wale wanaotumia mitandao ya jamii kuhimiza maandamano, kwamba wanajaribu kusambaza hofu na ghasia.

Baada ya wandamanaji wawili kuuwawa katika mji wa Dorud , wakuu wa huko walikanusha kuwa askari wa usalama walifyatua risasi.

Wamesema vifo hivyo vilitokana na wachochezi wanaowakilisha nchi za nje, na wachochezi wengine kati ya raia.

Nighttime photo shows fires in a Tehran street

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Moto uliwashwa wakati wa maandamano