Zimbabwe: Emmarson Mnangagwa '' Mamba'' atarajiwa kuiongoza

Emmerson Mnangagwa

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Bwana Mugabe anaonekana kuwa amekuwa akichezea hisia za Emmerson Mnangagwa(pichani) akimpandisha na kumshusha vyeo vya Chama tawala cha ZANU-PF na serikalini

Ni siri iliyofichuka nchini Zimbabwe kwa miaka mingi kwamba Emmerson Mnangagwa alitaka kumrithi Robert Mugabe kama rais.

Na Bwana Mugabe anaonekana kuwa amekuwa akichezea hisia zake - na amekuwa akimpandisha vyeo katika chama tawala cha Zanu-PF party na hata katika serikali, jambo lililozusha uvumi kwamba Bwana Mnangagwa ''ndie mrithi wake'' lakini baadaye alimshusha cheo huenda baada ya kuonyesha azma yake wazi pengine kupita kiasi.

Lakini baada ya kufutwa kazi, inaonekana kana kwamba subra ya Mnangagwa anayefahamika kwa jina maarufu la "mamba" ilikwisha.

Baada ya kufutwa kazi na Bwana Mugabe kumpuuza na kumshutumu hadharani kwa "usaliti", wafuasi wake katika jeshi waliingilia kati kwa niaba yake.

Lakini yeyote mwenye matumaini kwamba urais wa Mnangagwa utamaliza ukiukaji wa haki za binadamu nchini Zimbabwe huenda anajitanganya .

Bwana Mnangagwa (kushoto) akiwa pamoja na rais Mugabe

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Bwana Mnangagwa (kulia) amekuwa akikabiliwa na mabadiliko katika maisha yake ya kisiasachini yau tawala wa rais Mugabe

Wakosoaji wake wanasema kuwa Kiongozi huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 71- ana damu mikononi mwake.

uhusiano wake na Kongo

Bwana Mnangagwa alizaliwa katika jimbo la Zvishavane na anatoka katika kabila dogo ambalo ni sehemu ya jamii ya Washona

Watu wa Kabla la Karanga ni kabila kubwa katika jamii ya Washona na baadhi wanahisi ni wakati wao sasa wa kuingia madarakani, kufuatia miaka 37 ya utawala wa raia Mugabe anayetoka katika kabila la Zezuru