Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Macron aitaka Libya kuwakabili wahamiaji haramu kwa kuwapa mahitaji maalum
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ametoa mapendekezo ya kuweka vituo nchini Libya ili kutekeleza mahitaji ya raia wanaomba hifadhi nje ya taifa hilo.
Hatua hiyo ni kufuatia Italia kuonyesha mashaka katika jambo hilo.
Macron amesema kuwa mradi huo utaanza kutekelezwa ndani ya miezi miwili ijayo.
Lakini Waziri mkuu wa Italia ,Paolo Gentiloni, amesema kuwa tatizo la ukimbizi haliwezi kutatuliwa kwa njia ya kuwaondoa nchini humo.
Umoja wa jumuiya ya Ulaya inapaswa kuchukua hatua ambazo zitaipatia uwezo Libya kuleta hali ya Amani.
Gentiloni pia amesema kuwa wiki ijayo wanatarajia kuwasilisha muswada bungeni utakaowapa mamlaka Italia kutumia vyombo vya majini kukabiliana na wahalifu ndani ya Libya.