Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Italia kuzuia kuingia kwa wahamiaji katika pwani zake
Italia imetishia kuzuia meli za mataifa mengine kuwashusha wahamiaji katika bandari yake.
Mwakilishi wa taifa hilo katika jumuiya ya mataifa ya bara Ulaya, Maurizio Massari, ameonya kuwa idadi ya wahamiaji wanaovuka bahari ya Mediterranea kutoka Afrika kaskazini inazidi kuongezeka.
Karibu watu elfu kumi wameripotiwa kujaribu safari hiyo siku chache zilizopita.
Awali kamisheni wa masuala ya ihamiaji katika EU, Dimitris Avramopoulos, alisema mataifa yote wanachama wa jumuiya ya Umoja wa Ulaya yalikuwa na jukumu la kibinadamu kuokoa maisha na kwamba hayangeweza kuachia jukumi hilo mataifa machache kakabiliana na suala hilo.
Mataifa ishirini na nane wanachama wa jumuiya hiyo wametoa chini ya nusu ya Euro milioni mia mbili waliyokuwa imeahidi kukabiliana na wahamiaji barani Afrika hususan Libya ambayo ndio kituo kikuu cha mwanzo wa safari.