Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Waandamanaji wajenga ukuta kuwazuia wahamiaji Ufaransa
Waandamanaji katika mji ulio kusini magharibi mwa Ufaransa wamejenga ukuta unaozunguka lango la hoteli ya zamani kuzuia isitumiwa kama makao ya wahamiaji.
Wakaazi kadha waliweka ukuta wenye umbali wa mita 18 na urefu wa mita 1.8 unaozunguka hoteli ya Formule 1.
Walisema kuwa mamlaka zimeshindwa kujadili na wakaazi wa mji mipango ya kuwapa makao wahamiaji hao 85.
Mamlaka bado hazijasema lolote kuhuhu ujenzi wa ukuta huo.
Waandamanaji walifanya kazi hadi usiku kuweka ukuta huo.
"Hatupingi kuwachukua waandamanaji lakini lazima suala hili liwajibikiwe," msemaji wa kundi hilo Laurent Teixeira, alisema.
Walionya kuwa mji huo mdogo wenye watu 5,500 hauna uwezo kuwachukua wahamiaji hao.