Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Urusi kuwatimua wanadiplomasia 30 wa Marekani
Urusi iko tayari kuwatimua wanadiplomasia 30 wa Marekani na kutwa mali ya Marekani kujibu vikwazo vya Marekani, kwa mujibu wa maafisa wa Urusi.
Vitisho hivyo vinatolewa kutoka wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ya Urusi na kunukuliwa na gazeti la daily Izvesta.
Mwezi Disemba utawala wa Obama uliwatimua wanadiplomasia 35 wa Urusi na kufunga makao mawili ya kijasusi.
Hatua hizo ni jibu kwa madai ya kuwa Urusi iliingilia uchaguzi wa Marekani.
Urusi tayarai iko chini ya vikwazo vya Marekani.
Timu ya Trumo hayo iko chini ya uchunguzi kufuatia madai ya Urusi kuingia kati kampeni ya mwaka uliopita. Hata hivyo Urusi imekana madai hayo.