Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Trump na Putin kupunguza migogoro duniani
Rais wa Marekani na Urusi wameongea kwa njia ya simu kujadili namna ya kushughulikia migogoro mbalimbali inayoikabili dunia kwa sasa.
Taarifa kutoka ikulu ya marekani zinasema kuwa Donald Trump na Vladimir Putin wamekubaliana kuwa vita vinavyoendelea Syria vimefikia katika hatua mbaya na pande zinazohasimiana hazina budi kukaa pamoja na kumaliza mapigano hayo.
Viongozi hao wawili pia wamejadili namna ya kufanya kazi kwa pamoja kuliangamiza kundi la IS pamoja na suala la nyuklia la Korea ya Kaskazini.
Haya ni maongezi ya kwanza kwa viongozi hao wawili, tokea Trump alipoishambulia Syria inayoingwa mkono na Urusi.