Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Vladmir Putin: Donald Trump ni mtu hodari
Rais Vladmir Putin amemsifu rais mteule wa Marekani, Donald Trump, kuwa mtu hodari, ambaye atazowea haraka majukumu yake mapya.
Akihojiwa katika televisheni ya Urusi, rais Putin alisema mafanikio yake katika biashara, yanaonesha kuwa Bw Trump ana akili, na kwamba Urusi inaona atachukua hatua kufuatana na hayo.
Kiongozi wa Urusi amesema siasa za dunia zinabadilika, na kwamba Urusi italinda maslahi yake na kuheshimu maslahi ya wengine.