Polisi wakamata watu 12 kufuatia shambulizi la London

Chanzo cha picha, Getty Images
Polisi mjini London, wanasema wamewakamata watu 12, katika maeneo tofauti mtaa wa Barking, mashariki mwa jiji, kuhu-siana na shambulio katika Daraja la London, ambapo watu 7 waliuwawa, na 48 kujeruhiwa.
Polisi wanasema wanaendelea kufanya msako katika eneo hilo,.
Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May, anasema uchaguzi mkuu wa Alhamisi, licha ya kutokea shmbulizi la tatu katika muda kama huo.

Chanzo cha picha, AFP
Alisema ghasia zisiruhusiwe kuchafua utaratibu wa demokrasi.
Alielezea shambulio hilo, kuwa msimamo unapotosha Uislamu na ukweli.
Watu 21 wako katika hali mahututi.

Chanzo cha picha, Reuters









