Afghanistan yaomboleza shambulizi la Taliban ambapo zaidi ya wanajeshi 100 waliuawa

Afghanistan inaomboleza kitaifa baada ya mauaji yaliyofanywa na Taliban Ijumaa, katika kambi ya jeshi, karibu na mji wa Mazar-i-Sharif, kaskazini mwa nchi.

Wakuu wanasema wanajeshi kama 140 waliuawa wakati wapiganaji walipovamia kambi hiyo, huku wakifyatua risasi wakati wanajeshi wanatoka msikitini na wale waliokuwa mkahawani.

Msemaji wa Taliban alielezea shambulio hilo kuwa la kulipiza kisasi, kwa viongozi wao waliouwawa hivi karibuni.

Maafisa wanasema kuwa kuwa idadi ya wanajeshi waliouawa huenda ikafikia 140