Mshauri wa Trump alitaka Fethullah Gulen kuondolewa Marekani

Chanzo cha picha, Reuters
Aliyekuwa mshauri wa maswala ya kiusalama wa rais wa Marekani Donald Trump ,Michael Flynn alizungumza kuhusu kumuondoa kiongozi wa dini aliye mafichoni Marekani anayesakwa na Uturuki kulingana na aliyekuwa mkurugenzi wa idara ya ujajusi James Woolsey.
Uturuki inamshtumu kiongozi huyo wa dini Fethullah Gulen kwa kuandaa mapenduzi ya mwaka uliopita nchini Uturuki.
Katika mahojiano yalirekodiwa katika kanda ya video Bwana Woolsey aliambia jarida la Street Jaournal alikuwa katika mazungumzo kuhusu njia za kumuondoa kiongozi mbali na hatua halali za kisheria.
Hatahivyo Bwana Flynn amekana madai hayo ya Whoolsey.
Mkutano huo ulifanyika mnamo mwezi Septemba katika hoteli moja mjini New York.
Wale waliohudhuria mazungumzo hayo ni pamoja Flynn wakati huo akiwa mshauri wa bwana kampeni ya bwana Trump kuhusu maswala ya kiusalama, mwana wa kambo wa rais wa Uturuki Tayyip Erdogan pamoja na waziri wa maswala ya kigeni nchini Uturuki Mevlut Cavusoglu kulingana na jarida la Wall Street Journal.

Chanzo cha picha, AP
Bwana Woolsey ambaye pia alikuwa mashauri wa kundi la kampeni la Trump alikiri kwamba alichukua tahadhari kwa sababu aliwasili kuchelewa katika mkutano huo.
Lakini aliambia jarida hilo kwamba kuliwa na mazungumzo mazito kuhusu kutafuta njia za kumfurusha bwana Gulen kutoka Marekani na kumpeleka Uturuki.
''Unaweza kusema ulikuwa mkutano wa kutafuta mbinu, lakini ulikuwa unaangazia swala zito ambalo lilikuwa linakiuka sheria''.












