Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kashfa ya mahindi yamfuta kazi waziri Malawi
Waziri wa kilimo nchini Malawi George Chaponda amefutwa kazi kufuatia kashfa ya ufisadi inayoitwa 'Maizegate'.
Mwezi uliopita Rais Mutharika aliagiza uchunguzi kuhusu agizo la ununuzi wa mahindi yenye thamani ya dola milioni 34.5 kutoka Zambia.
Inadaiwa kuwa kiwango fulani cha mzigo huo kilitoweka mbali na fedha zilizotolewa kununua bidhaa hiyo.
Bwana Chaponda aliambia BBC wiki iliopita kwamba hataondoka afisini hadi atakapopatikana na hatia ya makosa yoyote swala alilokana.
Waziri wa habari Nicolaus Dausi aliambia chombo cha habari cha Reuters kwamba:
''Rais amemuondoa katika baraza la mawaziri mheshimiwa George Chaponda kuwa waziri wa kilimo mara moja baada ya kupatikana na mamilioni ya fedha katika nyumba yake hapo jana'.