Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Netanyahu akana kashfa ya ufisadi inayomkabili
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amekana kufanya makosa yoyote kufuatia madai ya ufisadi yanayomkabili katika vyombo vya habari.
Kumekuwa na madai kwamba alipokea zawadi kinyume na sheria kutoka kwa wafanyibiashara, na kwamba mwanasheria mkuu wa taifa hilo anatarajiwa kuanzisha uchunguzi.
Lakini katika taarifa yake Netanyahu amesema kuwa uchunguzi huo utafeli kupata ushahidi wowote dhidi yake.
Amesema kuwa hakuna chochote cha kuficha.