Nigeria ndiyo ya tatu kuathiriwa vibaya na ugaidi duniani

Wanamgambo wa Boko Haram

Chanzo cha picha, AFP/GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Wanamgambo wa Boko Haram

Nigeria ndiyo nchi ya tatu duniani kati ya nchi zilizoathiriwa vibaya na ugaidi baada ya Iraq na Afghanistan.

Somalia ilichukua nafasi ya saba kati ya nchi zilizoathirika zaido na ugaidi baada ya Pakistan, Syria na Yemen.

Idadi yote ya watu waliouawa kutokana na ugaidi ilipungua kwa asilimia 10 mwaka uliopita hasa kutokana na oparesheni za kijeshi dhidi ya wanamgambo wa Boko Haram nchini Nigeria na kundi la Islamic State nchini Iraq.

IS lilishinda Boko Haram kama kundi hatari zaidi la kigaidi mwaka 2015

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, IS lilishinda Boko Haram kama kundi hatari zaidi la kigaidi mwaka 2015

Lakini licha ya mwaka 2015 kushuhudia vifo 29,376, bado ulisalia kuwa mwaka hatari zaidi katika historia.

IS lilishinda Boko Haram kama kundi hatari zaidi la kigaidi mwaka 2015 kwa kufanya mashambulizi kwenye miji 252 ambapo watu 6,141 waliuawa.

Idadi ya watu waliouawa na Boko Haram ilipungua kwa asilimia 18. Kundi hilo lilihusika na vifo 5,478 mwaka 2015.

Hata hivyo Boko Haram na IS bado ni tisho kubwa baada ya makundi hayo kuenea kwenda nchi zingine.