Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
UN yawasaidia wapiganaji wa Machar DR Congo
Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wanaolinda Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanasema wamesaidia kuwasafirisha zaidi ya wapiganaji 100 kutoka Sudan Kusini hadi vituo vya afya nchini DRC kupokea matibabu.
Msemaji wa UN Stephane Dujarric amesema wapiganaji hao, watiifu kwa kiongozi wa waasi Riek Machar, walikuwa katika hali mbaya kiafya walipowasili nchini humo.
Bw Machar mwenyewe alipewa usaidizi wa kimatibabu na wanajeshi wa UN baada ya kujeruhiwa mwezi uliopita katika mapigano nchini Sudan Kusini.
Baadaye aliondoka DRC na kuelekea Sudan. Alitibiwa kwa muda na kuruhusiwa kuondoka hospitalini mwishoni mwa mwezi Agosti ingawa bado amesalia nchini Sudan.