Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Riek Machar atibiwa Sudan baada ya kutoroka Sudan Kusini
Wasaidizi wa kiongozi wa upinzani nchini sudan Kusini , Riek Machar, wanasema kwamba ameruhusiwa kuondoka hospitalini nchini Sudan japo ataendelea kuishi nchini humo.
Bwana Machar alikuwa akitibiwa mguu wake uliokuwa umevimba,kutokana na majeraha iliyopata wakati akitoroka kutoka Sudan Kusini.
Machar anatarajiwa kukutana na rais Omar al-Bashir hivi karibuni.
Machar alifutwa kazi kama makamu wa rais baada ya vita kuzuka upya Sudan Kusini.
Wanajeshi watiifu kwake walianza kupigana na wanajeshi watiifu kwa hasimu wake wa kisiasa rais Salva Kiir.
Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan Kusini vilizuka tena Desemba 2013 kufuatia jaribio la kupindua serikali.
Mapigano yaliendelea hadi kutiwa saini kwa mkataba wa Amani Agosti mwaka jana.
Lakini katika miezi ya hivi karibuni, vita vimezuka upya na aliyekuwa makamu wa rais kuambatana na mkataba huo wa amani, Dkt Riek Machar, akaondoka mji mkuu Juba.