Watoto wanavyonyanyaswa kingono katika migodi haramu ya Afrika Kusini

Chanzo cha picha, Getty Images
- Author, Mayeni Jones
- Nafasi, BBC News, Johannesburg
- Muda wa kusoma: Dakika 5
Taarifa hii ina maelezo na video ambayo huenda ikawaathiri baadhi ya wasomaji.
Kitu kilichomstaajabisha sana Jonathan, ambaye aliishi na kufanya kazi ya kuchosha kwa miezi sita chini ya ardhi ya mgodi wa dhahabu uliotelekezwa nchini Afrika Kusini, ni unyanyasaji alioshuhudia ukitendewa watoto.
Baadhi yao hufanya kazi ya vibarua kwa malipo kidogo, lakini wengine huletwa kwa ajili ya ngono, wanaharakati wanasema.
Jonathan, ambaye sasa ana umri wa miaka 20 hivi, alihamia Afrika Kusini kwa matumaini ya kujikimu kimaisha kwa kufanya kazi katika mojawapo ya migodi yake mingi ikiwa ni pamoja na zile zilizofungwa na mashirika ya kimataifa kwa sababu hazikuwa na faida tena kwa biashara.
Tunalinda utambulisho wake kwa hiyo hatutatumia jina lake halisi kwani anahofia kuvamiwa na magenge ya uhalifu yanayoendesha shughuli ya uchimbaji haramu wa madini kwa kuzungumza na vyombo vya habari.
Kwa sauti ya upole, anaelezea kazi aliyofanya kwa muda mrefu katika mazingira magumu bila ya kuwa na chakula cha kutosha na uhaba wa usingizi ulivyoathiri afya yake.
Lakini kumbukumbu ya kudumu ni kile kilichowakabili wachimbaji wadogo kwenye mgodi ambapo alifanya kazi.
"Nilikuwa nikiwaona watoto hawa kwenye mgodi - vijana, wenye umri wa miaka kati ya 15 hadi 17.
"Wakati mwingine baadhi ya watoto hao walikuwa wakitumika vibaya. Ilikuwa ni hali ya kutisha na kusikitisha."
Alisema wachimbaji madini watu wazima walikuwa wakibaka kwa ahadi ya kuwapa baadhi ya dhahabu walizozipata.
"Ikiwa mtoto hana jinsi anashawishika kushiriki vitendo hivyo viovu."
Jonathan anaelezea jinsi baadhi ya watoto wangewaomba wachimbaji madini kuwapa ulinzi lakini ''ombi lao linakubaliwa kwa masharti."
Ngono pia ilitumiwa kama adhabu ikiwa vijana walishindwa kukamilisha kazi kwa walizopewa.
Jonathan anasema watoto katika mgodi aliofanya kazi wote walikuwa wageni na hawajua kile ambacho kilikuwa kinawasubiri.

Chanzo cha picha, AFP
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Mtafiti na mwanaharakati wa madini Makhotla Sefuli anaunga mkono hili.
Anasema magenge ya wahalifu yanalenga hasa watoto kufanya kazi katika migodi haramu kote Afrika Kusini.
Wengi wao hutekwa nyara kutoka nchi jirani na kuletwa nchini humo. Wanashawishiwa na ahadi zisizo na msingi za kuwatafutia ajira katika sekta rasmi ya madini.
"Wanapokonywa paspoti zao wanapofika Afrika Kusini... Sula la kunyanyaswa kwa wavulana hawa wadogo linajulikana wazi," Bw Sefuli anasema.
BBC imezungumza na wachimbaji madini waliokuwa wakifanya kazi katika migodi mingine miwili isiyo halali ambao walikiri kuwaona watoto wakinyanyaswa kwenye migodi walimokuwa wakifanya kazi.
Tshepo, sio jina lake halisi, anasema aliona wanaume wakiwalazimisha wavulana wadoho kufanya nao mapenzi kwa siri.
"Katika baadhi ya matukio, walifanya hivyo kwa ajili ya pesa. Wengine wanapewa ajira kwa ajili hilo tu kwa maslahi ya kifedha ambayo hutokana na kufanya biashara ya ngono."
Anaongeza kuwa unyanyasaji huo uliwaathiri sana watoto.
"Wanabadilisha mienendo yao na kuzingatia zaidi uaminifu. Hawataki uwe karibu nao, kwa sababu wanahisi kwamba hawawezi kumwamini mtu yeyote tena."
Maelezo ya kile ambacho vijana hao walikuwa wakikumbana nayo yalitokana na mvutano kati ya polisi na maelfu ya wachimba midini haramu mwishoni mwa mwaka jana nchini Afrika Kusini.
Matukio katika mgodi wa dhahabu wa Buffelsfontein, karibu na mji wa Stilfontekatika Mkoa wa Kaskazini Magharibi yaligonga vichwa vya habari kimataifa wakati taarifa ya operesheni ya usalama ilipoibuka.
Mamlaka ilikuwa ilikuwa ikijaribu kudhibiti uchimbaji madini haramu ambao serikali ilisema uligharimu uchumi wa Afrika Kusini takribani dola bilioni 3.2 za Kimarekani mwaka jana.
Walianzisha operesheni inayoitwa Vala Umgodi, au kuziba shimo hilo, mnamo Desemba 2023, na kuahidi kuchukua mhatua kali dhidi ya magenge ya uhalifu.
Kama sehemu ya operesheni hiyo, polisi walipunguza kiwango cha chakula na maji ambacho kilishuka kwenye mgodi wa Stilfontein ili, kama waziri mmoja alivyosema, "kuwashinikiza" wachimbaji haramu kutoka chini ya ardhi. Maafisa walisema watu hao walikuwa wakikataa kutoka kwenye mgodi huo kwa kuhofia kukamatwa.
Haikuchukua muda picha zinazoashiria hali ngumu wanayopitia wachimbaji hao zikaanza kuibuka. Makumi ya wanaume waliodhoofika walionekana wakiomba kuokolewa wakiwa na mabegi yao. Hatimaye mahakama iliamuru serikali kuwaokoa watu hao.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa YouTube ujumbe
Miongoni mwa waliookolewa walikuwa watato wavulana walio na umri mdogo, lakini kwa kuwa wengi wao walikuwa wahamiaji bila hati za kuthibitisha umri wao, mamlaka iliwafanyia vipimo vya afya ili kukadiri umri wao.
Kupitia hili, Idara ya Maendeleo ya Jamii (DSD) ilithibitisha kuwa wachimbaji 31 kati ya waliookolewa katika mhodoi wa Stilfontein walikuwa watoto. Wote walikuwa raia wa Msumbiji na baadhi yao walirejeshwa makwao mnamo Novemba, 27 mwaka jana.
Shirika la Save the Children la Afrika Kusini lilisaidia kutafsiri baadhi ya mahojiano kati ya wachimba midini waliokuwa na umri mdogo na waokoaji.
"Wanakabiliwa na kiwewe, kwa sababu baadhi yao pia walishuhudia wenzao wakinyanyaswa kingono," Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la misaada Gugu Xaba aliambia BBC.
"Hofu kwamba huenda wasinusurike ziliwaathiri watoto hao kiakili.
"Wachimba midini watu wazima wangeanza kwa kuwatunza, kwa kufanya kama wanavyowapenda."
Anasema watoto hao walilazimishwa kufanya ngono na watu wazima na kisha kubakwa siku baada ya siku.
"Unakuta kwamba mtu mzima atakuwa na watatu au wanne kati yao ambao wanafanya kitu kimoja."

Bi Xaba anasema magenge ya wachimbaji madini huajiri watoto kwa sababu ni rahisi kuwadhibiti kwa kibarua cha bei nafuu.
"Watoto hawaelewi unaposema: 'Nitakulipa randi 20 ($1; £0.80) kwa siku.' Watu wazima wakati mwingine hukataa kufanya kazi, lakini watoto hujikuta hawana budi, kwa hivyo ni rahisi kumchukua mtoto ambaye hawezi kujieleza na kumleta huko.
Zaidi ya kunyonywa kifedha, anasema kuna magenge ambayo yanasajili watoto na kuwarubuni kwa ngono.
Baadhi ya wachimbaji madini haramu huishi kwa miezi kadhaa miezi chini ya ardhi, hubuka kutoka kwa amshimohayo wanapopata soko la kuuza bidhaa zao na huwapatia chochote wanachohitaji.
"Watoto wengi wanasafirishwa ili watumike kama watumwa wa ngono. Kuna mtu ambaye ananufaika kifedha, na hii inamaanisha kila siku mtoto huyu anatumika kama mfanyabiashara ya ngono."
BBC iliuliza polisi ikiwa kuna mtu yeyote atayeshtakiwa kwa madai ya unyanyasaji wa kingono lakini haikupata jibu ya swali hilo.
Chanzo kinachoshughulikia kesi za wachimba midini wa Stilfontein kilisema baadhi ya watoto hawakutaka kutoa ushahidi.
Wakati huo huo, sekta haramu ya madini inaendelea kustawi.
Huku ikikadiriwa kwamba kuna migodi 6,000 iliyo wazi ambayo bado inachunguzwa, kuna uwezekano biashara hii haramu huenda isikomweshwe hivi karibuni na hali hii inawaacha hatarini maelfu ya watoto.
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi












