Wanyanyasaji wa watoto kingono wanavyotumia Akili Mnemba (AI)kugeuza waimbaji na nyota wa filamu kuwa watoto

Chanzo cha picha, Getty Images
Na Joe Tidy
Mwandishi wa Usalama wa Mtandao
Wanaowanyanyasa watoto kingono wanatumia akili ya bandia/Akili mnemba (AI) kuunda picha za watu mashuhuri wakiwa watoto.
Wakfu wa Internet Watch (IWF) ulisema kwamba picha za mwimbaji mashuhuri wa kike aliyeibuliwa upya akiwa mtoto zinashirikiwa na washukiwa hao .
Katika jukwaa moja la mtandao wa siri shirika hilo la hisani linasema picha za waigizaji wakiwa watoto pia zinabadilishwa ili kuwafanya wafanye ngono.
Mamia ya picha za waathiriwa halisi wa unyanyasaji wa kingono kwa watoto pia sasa zinaundwa kwa kutumia jenereta za picha zilizowekwa wazi.
Maelezo yanatoka kwa ripoti ya hivi punde zaidi ya IWF kuhusu tatizo linaloongezeka, inapojaribu kuongeza ufahamu kuhusu hatari za washukiwa hao kutumia mifumo ya AI ambayo inaweza kuunda picha kutoka kwa maagizo rahisi ya maandishi.
Tangu mifumo hii yenye nguvu ya kutengeneza picha iingie kwa umma, watafiti wameonya kuwa ina uwezo wa kutumiwa vibaya kutengeneza picha haramu.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Mwezi Mei, Waziri wa Mambo ya Ndani Suella Braverman na Waziri wa Usalama wa Ndani wa Marekani Alejandro Mayorkas walitoa taarifa ya pamoja ya kukabiliana na "ongezeko la kutisha la picha za kuchukiza zinazozalishwa na AI za watoto wanaonyanyaswa kingono na washukiwa hao.
Ripoti ya IWF inaeleza jinsi watafiti walivyotumia mwezi mmoja kutafuta picha za AI kwenye tovuti moja ya unyanyasaji wa watoto kwenye mtandao wa wa siri na walipata karibu picha 3,000 za maandishi ambazo zingekuwa kinyume cha sheria kwa mujibu wa sheria za Uingereza.
Wachambuzi walisema kuna mtindo mpya wa wahalifu hao kuchukua picha moja za waathiriwa wanaojulikana wa unyanyasaji wa watoto na kuziunda tena nyingi zaidi katika mazingira tofauti ya unyanyasaji .
Folda moja waliyopata ilikuwa na picha 501 za mwathiriwa wa ulimwengu halisi ambaye alikuwa na umri wa miaka 9-10 alipodhulumiwa kingono. Katika folda washukiwa hao walishiriki faili ya muundo wa AI iliyosasishwa vizuri ili kuruhusu wengine kutoa picha zao zaidi.
IWF inasema baadhi ya picha , ikiwa ni pamoja na zile za watu mashuhuri wakiwa watoto, halisi kabisa na haiwezi kutofautishwa na mtu asiye na ujuzi wa kuzitofautisha.
Wachambuzi waliona picha za waimbaji wengi wa kike na nyota wa filamu ambao walikuwa wamepunguzwa umri kwa kutumia programu ya upigaji picha ili kuwafanya waonekane kama watoto.
Ripoti hiyo haikubainisha ni watu gani maarufu waliokuwa wakilengwa.
Shirika hilo lilisema lilikuwa linashiriki utafiti ili kuliweka suala hilo kwenye ajenda katika Mkutano wa AI wa serikali ya Uingereza wiki ijayo huko Bletchley Park.
Katika mwezi mmoja, IWF ilichunguza picha 11,108 za AI ambazo zilishirikiwa kwenye jukwaa la unyanyasaji wa watoto kwenye tovuti.
Kati ya hizi, 2,978 zilithibitishwa kama picha ambazo hazifuati sheria za Uingereza - ikimaanisha zilionyesha unyanyasaji wa kijinsia wa watoto
Zaidi ya picha moja kati ya tano kati ya hizi (564) ziliainishwa kama Kitengo A, aina mbaya zaidi ya picha za unyanyasaji.
Zaidi ya nusu (1,372) ya picha hizi zilionyesha watoto wenye umri wa shule ya msingi (umri wa miaka saba hadi 10)
Pamoja na hii, picha 143 zilionyesha watoto wenye umri wa miaka mitatu hadi sita, wakati picha mbili zilionyesha watoto (chini ya miaka miwili).
Mwezi Juni, IWF ilionya kwamba wahalifu hao walikuwa wanaanza kuchunguza matumizi ya AI kutengeneza picha potovu za watoto, lakini sasa IWF inasema hofu hiyo ni ukweli.
"Hofu yetu mbaya zaidi imetimia," alisema Susie Hargreaves, mtendaji mkuu wa IWF.
"Mapema mwaka huu, tulionya picha za AI hivi karibuni zinaweza kukosa kutofautishwa na picha halisi za watoto wanaonyanyaswa kingono, na kwamba tunaweza kuanza kuona taswira hii ikiongezeka kwa idadi kubwa zaidi. Sasa tumepita hatua hiyo."
Ripoti ya IWF inakariri madhara halisi ya ulimwengu wa picha za AI. Ingawa watoto hawadhuriwi moja kwa moja katika uundaji wa maudhui, picha hizo hurekebisha tabia ya unyanyasaji na zinaweza kupoteza rasilimali za polisi wanapochunguza watoto ambao hawapo.
Katika baadhi ya matukio aina mpya za makosa zinachunguzwa pia, na kuibua mambo magumu mapya kwa mashirika ya kutekeleza sheria.
Kwa mfano, IWF ilipata mamia ya picha za wasichana wawili ambao picha zao kutoka kwa wakala wa uanamitindo wasio wa picha za utupu ambazo zilikuwa zimewekwa a katika matukio ya unyanyasaji wa kijinsia ya Kitengo A.
Ukweli ni kwamba sasa ni waathiriwa wa makosa ya Kundi A ambayo hayajawahi kutokea.















