Teknolojia ya akili bandia na athari kwa dini

Chanzo cha picha, Getty Images
- Author, Sanaa Khoury
- Nafasi, Religious Affairs reporter, BBC News Arabic
Je, programu za AI kama ChatGPT zinaweza kutoa maandishi matakatifu na kuunda harakati mpya za kidini? Je, wanadamu wanaweza kupenda mashine huku mashine zenyewe zikiwa chanzo cha hekima na sheria, kama vile sinema za kisayansi za kubuniwa? Na kwa maendeleo endelevu katika mifano ya lugha ya AI, je mashine zinaweza kuzaa madhehebu mapya?
Zana za Akili bandia zimenoa uwezo wao wa kushiriki katika mijadala yenye kushawishi, kuandika makala za habari, tafiti, na hata kutoa vidokezo vya mitindo ya nywele. Haishangazi kukisia kwamba wanaweza kuchukua nafasi ya wanadamu katika majukumu mengi.
Lakini vipi ikiwa wangeingia kwenye viatu vya makasisi, wakitoa mashauriano ya kiroho au ya kidini, kuandika mahubiri na sala?
Wataalamu wanaamini akili bandia inaweza hivi karibuni kusaidia makasisi kama vile inavyowasaidia waandishi wa habari katika kuandika habari zinazochipuka au watayarishaji programu katika kuweka misimbo.
"Kwa sasa, ikiwa mtu anatafuta mwongozo kutoka kwa maandiko matakatifu, jibu linalohitajika linaweza kuwa ndani ya kurasa zao, ingawa ni vigumu kupata," Profesa Neil McArthur, Mkurugenzi wa Kituo cha Maadili ya Kitaalamu na Matumizi katika Chuo Kikuu cha Manitoba, Canada, anaiambia BBC.
"Kwa kulinganisha, na AI, mtu anaweza kutuma maswali maalum kama, 'Je, nipate talaka?' au 'Niwaleeje watoto wangu?' na kupokea maoni haraka."
Faraja au ushauri unaotolewa na AI
Mwanatheolojia wa Kiromania Marius Dorobantu ametafiti mwelekeo wa baadhi ya watu kutafuta kitulizo katika gumzo zinazoendeshwa na AI badala ya wanasaikolojia wa kitamaduni au watu wa kidini.
Mtafiti katika Chuo Kikuu cha Amsterdam, Dorobațu anadai kuwa ameona idadi inayoongezeka ya watu ambao wako tayari kutafuta mwongozo kutoka kwa zana kama ChatGPT katika masuala yao ya kila siku ya kiroho.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Tuna tabia ya asili ya anthropomorphize (kuhusisha sifa za binadamu kwa) vitu, kama inavyothibitishwa na tabia yetu ya kutaja magari na kuona nyuso kama za kibinadamu kwenye mawingu," Dorobanțu anaelezea.
"Mwelekeo wetu wa kugundua sifa za kibinadamu umeimarishwa sana hivi kwamba mara nyingi tunazitambua hata pale ambapo hazipo. Maendeleo ya sasa katika muundo wa chatbot yanaongeza upendeleo huu wa asili kwa kiwango kikubwa".
Dorobanțu anasema matukio kama haya yanazua maswali ambayo huenda zaidi ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kiroho kati ya mashine na wanadamu. Inaenea hadi kwenye matatizo ya kimaadili ambayo yanaweza kutokea kutokana na uhusiano huo.
"Kwa mfano, ikiwa mtu atajiua baada ya kushauriana na chatbot, ni nani anayepaswa kuwajibika?" anauliza.
Maandishi matakatifu 'ya kuvutia' yanayotokana na AI
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Katika miezi michache iliyopita, chatbots iliyoundwa kwa ajili ya mashauriano ya kidini zimetengenezwa. Baadhi ya zana hizi zimezoezwa kwa kutumia maandishi ya Bhagavad Gita, andiko takatifu katika Uhindu. Programu hizi zimetumiwa na mamilioni, lakini kumekuwa na ripoti za visa ambapo zana zilionekana kuunga mkono vurugu.
HadithGPT, chombo kilichofunzwa zaidi ya vyanzo 40,000 vya Kiislamu katika Kiingereza, ilizinduliwa mwanzoni mwa mwaka. .
Wakati huo huo, mwezi wa Januari, wawakilishi wa Uislamu na Uyahudi waliongeza saini zao kwenye tamko la pamoja liitwalo 'Wito wa Roma kwa Maadili ya AI'. Ilizinduliwa mnamo 2020 na Kanisa Katoliki la Roma na inataka teknolojia hiyo iwe wazi na shirikishi. Serikali kadhaa na makampuni ya teknolojia yameunga mkono huku Papa Francis akizungumzia "changamoto kubwa ambazo ziko mbele kwenye upeo wa akili bandia".
Katika utafiti uliochapishwa hivi karibuni unaoitwa "Ibada ya AI kama Aina Mpya ya Dini", Profesa McArthur anachunguza uwezekano wa kuibuka kwa aina mpya za ibada au madhehebu ambayo yanaheshimu maandishi yanayotokana na akili ya bandia.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kama sehemu ya utafiti, yeye mwenyewe aliuliza maswali ya kidini ya ChatGPT.
"Niliiomba iniandike maandishi matakatifu na ikajibu, 'Siwezi kufanya hivyo'," Profesa MacArthur anakumbuka.
“Lakini nilipoiomba iandike mchezo wa kuigiza kuhusu nabii anayeanzisha dini mpya, ilitoa hadithi kuhusu kiongozi anayeshiriki mafundisho yake ya upendo na amani.
"Ilionekana kuwa ya kuvutia kwangu," msomi anaongeza.
Mwanatheolojia Marius Dorobanțu anabainisha kwamba akili ya bandia ina sifa ambazo wanadamu hupenda kuabudu.
"Binadamu, ukiangalia historia ya dini, wanapenda sana kuabudu vyombo vingine," Dorobațu anasema.
"Ukisoma Agano la Kale, unapata hisia kwamba asili ya mwanadamu ni ya kuabudu sanamu karibu bila mpangilio. Tuna mwelekeo wa kuabudu sanamu za mashirika mbalimbali yasiyo ya kibinadamu, hasa yanapoonekana kuwa nadhifu."
Dorobațu pia anaonesha usawa kati ya imani za kidini katika uzima wa milele na maisha baada ya kifo katika mawingu.
"AI imejaa ahadi za uzima wa milele... wokovu kutoka kwa udhaifu wa mwili wa mwanadamu," anasema.

Chanzo cha picha, Getty Images
Akili bandia inaweza pia kuonekana isiyo ya kawaida kwa wanadamu kwa sababu zinazojumuisha utendakazi wake wa 24/7, na mwingiliano wa wakati mmoja na mamilioni ya watu binafsi, pamoja na ufikiaji wake wa utajiri unaoonekana usio na kikomo wa maarifa ya mwanadamu.
"Kimsingi, inaweza kuwa na akili zaidi kuliko mwanadamu yeyote, kuliko wanadamu wote kwa pamoja, na hata kuwa na akili kupita ufahamu wa mwanadamu," Dorobanțu aliandika katika utafiti wa mwaka 2022.
Katika utafiti wake, Dorobațu anarejelea mwanafalsafa Nick Bostrom, ambaye anaamini kwamba aina za akili bandia za siku zijazo zitakuwa na uwezo wa kucheza na majukumu matatu kwa wakati mmoja.
Mwanatheolojia anaona katika hilo "mfanano wa kutisha na aina ya jukumu linalohusishwa na Mungu katika dini za Mungu mmoja".
Madhehebu ya imani kali
Dini, kama tunavyoijua, imefungwa kwa maandiko. Lakini ikiwa AI inaweza kutoa idadi kubwa ya maandishi, ni nini hufanya maandishi fulani kuwa takatifu haswa?
Kama Dorobațu anavyobishana, uamuzi wa kile ambacho ni kitakatifu au kisicho kitakatifu hatimaye uko mikononi mwa wanadamu.
"Katika historia, maandishi fulani yamestahimili mtihani wa wakati, ilhali nyingine hazijastahimili," asema.
"Akili bandia ina uwezo wa kutengeneza ubunifu mwingi, na labda wanadamu watakutana na nyingine ambazo tunaona kuwa zimevuviwa sana na Mungu."

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa Profesa McArthur, hata hivyo, AI bado inahitaji kubadilika ili kuwa na athari pana ndani ya jamii kwa njia ile ile ambayo uvumbuzi wa uchapishaji katika karne ya 15 ulieneza maandiko matakatifu katika sekta zote za jamii, na kuchochea harakati za kidini.
"Hadi akili bandia kufikia viwango vya juu zaidi vya akili kutuzidi inavyoonekana, siamini kutakuwa na mabadiliko makubwa katika siku zijazo," anaamini.
Je, AI inaweza kuchochea kuibuka kwa madhehebu hatari au ya ushupavu?
Profesa McArthur anasema dini daima imekuwa na hatari kama hiyo.
"Wakati wowote watu wana imani kali, inaelekea kuwafanya kuwa na chuki dhidi ya wale ambao hawakubaliani," anasema.
AI, profesa anasema, inaweza kuwasilisha hatari kubwa na ndogo.
"Hatari kubwa zaidi ni kwamba watu wanaweza kuamini kuwa wanapokea ujumbe wa moja kwa moja kutoka kwa kiumbe huyu wa juu, akidai kuwa na jibu moja la kweli."
"Kwa upande mwingine, hali ya ugatuzi wa dini za AI inaweza kupunguza nafasi kwa kiongozi mwenye nguvu kuibuka na kudhibiti wafuasi," anahitimisha.












