Unataka kumsahau mpenzi wako wa zamani? fuata hatua hizi

SOMSARA

Chanzo cha picha, SAMSARA RIELLY

Maelezo ya picha, Wakili wa Nigeria Aronke Omame.

Mshangao alioupata katika mahakama ya talaka ulisababisha Aronke Omame kubadili kazi na kuwa mshauri wa talaka.

Ulikuwa mwaka 1993, wakili wa masuala biashara Aronke Omame mwenye umri wa miaka 35 alipojifunza somo kuhusu kuvunjwa moyo, jambo ambalo lingebadilisha maisha yake.

Yuko mahakamani mjini Lagos, Nigeria, lakini kwa mara ya kwanza hamwakilishi mteja. Anamuunga mkono rafiki yake Mary (si jina lake halisi), ambaye wazazi wake wanatalikiana.

Aronke anasema kwamba mama yake na Mary anaendelea kumwangalia baba ya rafiki yake. Sio vizuri. Anainua shingo yake ili kumtazama.

Kisha, hakimu alipotoa mapumziko mafupi, Aronke anawatazama Mary na mama yake wakitembea kuelekea kwa baba. Mahakama iko kimya, macho yote kwa familia.

Mary na mama yake wanapiga magoti mbele ya baba. Huku wakiinamisha kichwa wanamsihi asiivunje familia.

Lakini baba yake Mary anainua kidevu chake na kwa hasira anaanza kuwalaani wao kwa sauti kubwa, mbele ya kila mtu.

Mfano wa wazazi

Ni 1967 na Aronke mwenye umri wa miaka 9 yuko nje kwenye uwanja wa michezo na marafiki zake wakati mkuu wa shule anamkaribia. Ni nadra kumuona mkurugenzi wakati wa kucheza. Kuna kitu kibaya. Anamjulisha kuwa baba yake anasubiri mlangoni kumchukua. Kuna kitu kimetokea.

Baba yake Aronke anamwambia kwamba hawarudi nyumbani, anakaa nyumbani kwa bibi yake kwa wiki chache. Na kwa kuwa nyumba ya bibi yake iko maili nyingi kutoka mjini, hakuna mtu atakayeweza kumpeleka shuleni.

Atakuwa huru baba yake anamwambia.

Yeye na mama yake watamtembelea, kwa sasa wana mambo ya faragha ya kujadili.

Wanahitaji muda peke yao. Aronke amechanganyikiwa, lakini alihisi kwamba huu sio wakati wa kuuliza maswali.

SOMSARA RIELLY

Chanzo cha picha, SOMSARA RIELLY

Aronke anacheza na binamu zake na kupika na bibi yake. Ni furaha kuwa na wiki chache nje ya shule. "Wakati huo familia ilikuwa ya jumuiya," Aronke aliambia BBC. "Nililelewa na mababu na mashangazi na wajomba. Wazazi wangu walipata msaada mkubwa.”

Wazazi wake walidumisha uhusiano mzuri na hawakosoani mbele ya watoto. Familia haijavunjika. kulikuwa na mtu si chini ya mmoja anayelala nyumbani.

"Nimejifunza kwamba uhusiano haudumu kila wakati, licha ya nia nzuri ya kila mtu. unajaribu kuwa mkali kati ya kila mmoja, lakini kumaliza mambo kwa heshima kutakusaidia zaidi," anasema Aronke.

Hakuwahi kujua kwanini ndoa ya wazazi wake iliisha, lakini haijalishi. Wakati wote wa utoto wake, anasisitiza, alikuwa na furaha. Walakini, somo lake linalofuata la mapenzi litakuwa chungu.

SOMSARA

Chanzo cha picha, SOMSARA RIESLLY

kukataliwa

Aronke ana umri wa miaka 18, akiwa katika shule ya sheria anavutiwa na rafiki yake wa kiume ambaye alibadilika na kuwa katika mahusiano ya kimapenzi naye. Kwa mara ya kwanza alipenda.Lakini kuna tatizo. Anataka wafanye mapenzi na yeye hayuko tayari. Anajaribu kufidia kwa njia zingine, uwepo wake, upendo na kwa hiari. Siku moja, anaenda nyumbani kwake ili kumshtukiza, na akamkuta akimbusu msichana mwingine.

"Niliumia moyoni. Nilitoka nje nikidhani atakuja kwa ajili yangu." Na hakufanya hivyo. Baada ya kimya cha siku nyingi anapokea barua. "Anasema kwamba amepata mtu na kwamba mimi si sehemu ya maisha yake tena."

Aronke anaishia kuumizwa kwa kukataliwa. ''Niliaibishwa. Nilihisi kama dunia inaniangukia". Hakwenda darasani kwa wiki mbili, analia kitandani na anaogopa kukutana naye. Alipendelea kukaa nyumbani.

Marafiki zake walimtembelea, wakimwambia kwamba kuna chaguo bora zaidi zinazomngoja katika dunia wa nje.

SOMSARA

Chanzo cha picha, SOMSARA RIELLY

Kisha siku moja, kama miujiza tu, hali yake iliimarika. Anataka kwenda kutembea na lazima amalize digrii yake ya sheria na awe na marafiki wa kufurahiya nao. Anatoka nje ya mlango na kurudi kwenye maisha kawaida.

Wiki hizo mbili za kujitenga zilimsaidia sana. Anaweza hata, baada ya muda, wakawa marafiki tena na huyo mpenzi wake.

"Ninafurahi nilibubujikwa na machozi," asema. "Kumlilia lilikuwa somo zuri."

Mwanamke aliyetawaliwa

Miaka 17 baada ya kukatishwa tamaa huko, katika chumba cha mahakama cha Lagos, Aronke anatazama kwa mshangao babake Mary akimlaani mke wake na bintiye aliyepiga magoti. "Nilikuwa nikirusha maneno ambayo hata siwezi kuyakumbuka. Niliyafuta akilini, yalikuwa ya kuchukiza," anasema. Muda mfupi kabla, Aronke alikuwa amepitia talaka yake mwenyewe, lakini haikuwa mbaya kama fedheha ya umma ambayo alikuwa ameona.

Anashangaa jinsi mwanamke mwenye umri wa miaka 60 anavyoweza kumpigia magoti mwanamume anayemnyanyasa waziwazi, akimsihi asimwache.

Kisha natambua. "Utamaduni unaunga mkono mwanamke kutawaliwa na mume wake. Ikiwa hakuweza kutambua hapo awali, nilifanya wakati huo," anakumbuka.

Kuongezeka kwa ulimwengu wa talaka kidigitali

Google inaonyesha kuwa utafutaji wa "kumaliza talaka" umeongezeka maradufu katika miaka mitano iliyopita na kwa zaidi ya mara tatu tangu 2012.

KeywordTool.io, chombo kinachopima maneno ya utafutaji kwenye mifumo mbalimbali, inasema kwamba Ireland imetafuta zaidi "jinsi ya kuachana na mchumba/mpenzi wako" katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, na kwamba Nigeria, Singapore, India, Australia, Kenya, Marekani na Uingereza ni miongoni mwa nchi 10 bora.

Kwenye TikTok, #breakup ina zaidi ya hashtag bilioni 21 na #gettingoverabreakup ina milioni 8.7.

Shirikisho International Coaching Federation, linasema kuwa kufundisha uhusiano, ambayo ni pamoja na kufundisha kuachana, sasa kuna thamani ya zaidi ya dola bilioni 1 kwa mwaka.

Wakili 'Sisi'

Aronke alikumbuka watu waliomwambia kwamba kuzingatia kazi yake kumesababisha ndoa yake mwenyewe kuvunjika.

Na ndoa ya wazazi wake ilipoisha, macho yote yalikuwa yamemgeukia mama yake, wakimuuliza angeweza kufanya nini ili mumewe aendelee kuvutiwa naye.

Jamii ilikuwa inawasukuma wanawake kubaki kwenye ndoa zisizo na furaha, hata za matusi bila kuwapa ramani ya jinsi ya kutoka na kuanza maisha yenye mafanikio na kuridhisha.

Kwa hiyo siku hiyo, alipokuwa akitoka katika chumba cha mahakama ambako ndoa ya mama Mary ingevunjwa kisheria, Aronke alifanya uamuzi. Angesaidia watu kumaliza uhusiano wao kwautu zaidi iwezekanavyo. Kwa miaka kadhaa iliyofuata, alijikita katika masomo ya sheria ya familia na ushauri wa mahusiano.

Marafiki zake walimpachika jina la "Sisi Mwanasheria". Sasa anaitwa: "wakili Sisi: mshauri wa talaka".

Mshauri wa talaka

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Mwaka 2022, hakuna siku ya kawaida kwa wakili Sisi.

Akiwa na zaidi ya miaka 40 ya taaluma ya sheria na zaidi ya 10 kama mkufunzi aliyeidhinishwa nyuma yake, huamka na kupata ujumbe kila siku kwenye Facebook , hasa kutoka kwa wanawake, wakitafuta usaidizi wa kumaliza uhusiano.

Sasa ni sehemu ya kikundi kinachoibuka cha washauri wa uhusiano, washauri ambao husaidia kukabiliana na uchungu wa kusitisha uhusiano. "Mshauri wa talaka anaweza kukusaidia kutazama nyuma kwa kujivunia juu ya kipindi cha maisha kisichoepukika na chungu," anasema.

"Ingawa mshauri wa uhusiano anaweza kukusaidia kuvutia mtu mwingine, mshauri wa talaka hukusaidia kuwa mtu wa kujipenda wewe mwenyewe tena."

Ni biashara ambayo ipo nyuma ya pazia lenye siri.

“Ninapata jumbe kutoka kwa watu ambao hawanifuatilii waziwazi kwenye mitandao ya kijamii, jambo linaloashiria kwamba bado kuna aibu katika kusitisha uhusiano,” anasema. Lakini hakika inaonekana kuna soko la kusaidia kuyashinda mapigo ya moyo.

Aronke hutoza takriban $366 kwa vipindi vitatu. Mwanzoni, huwapa wateja wake mfumo wa kurudisha maisha yao kwenye mstari. Wiki mbili za kwanza ni muhimu, anasema. Anawahimiza wateja wake kulia, kuacha kumfuatilia au kuzima kitufe cha ujumbe wa mpenzi wako wa zamani kwenye mitandao ya kijamii, na kumwomba rafiki anayemwamini awasaidie kuwazuia wasichukuesimu ili wakupigie.

“Akili yako itakuchezea kwa visingizio vya kwa nini unahisi unahitaji kumpigia simu,” asema. "Puuza, anakudanganya. Ikibidi, mpe rafiki yako simu."

Badilisha jina la mpenzi wako wa zamani.

Kidokezo kisicho cha kawaida zaidi ni kubadilisha jina la mpenzi wako wa zamani unapozungumza kumhusu. "Ikiwa jina lake ni Steven, mwite Robert wakati unazungumza kuhusu yeye. Unaweza kuwa na hasira kidogo na Robert."

Kisha Aronke anawaelekeza wateja wake jinsi ya kupanga mikakati ya safari ndefu. "Pesa na mali mara nyingi huchanganywa katika mahusiano na huhitaji kutenganishwa. Ni ngumu na watu wanahitaji msaada katika hilo." Anasaidia wanawake kupitia upya fedha zao na bajeti ili wawe peke yao. Wakili Sisi anapokea shutuma mtandaoni kutoka kwa watu wanaosema: “Bila shaka mwanamke huyu anataka kuvunja familia, ni mwanamke aliyetalikiwa”.

Haikusumbui. Ana mpenzi lakini asingemuathiri hata angekuwa hana. Wakati mwingine kupoteza uhusiano ni wito wa kuamka ili kujifunza jinsi ya kujenga mahusiano bora katika siku zijazo."

Ushauri

Kwa muhtasari, wakili Sisi anapendekeza:

  • Lia.. Kulia husaidia kuondoa maumivu
  • .Usimpigie simu au kumtumia meseji mpenzi wako mliyeachana kwa angalau wiki kadhaa.
  • Mgeukie rafiki au mwanafamilia ambaye unaweza kuwasiliana naye mara kwa mara.
  • Kumbuka kwamba unahuzunika, na ndivyo pia hata kwa mpenzi wako mliyeachana. Huzuni ni kipindi cha marekebisho.
  • Mpe jina jipya mpenzi mliyeachana : Ikiwa jina lake ni Steven, mwite Robert huku ukimzungumzia, inaweza kukufanya upunguze hasira.
  • Acha kumfuatilia kwenye mitandao ya kijamii: Huu si wakati wa kujaribu kujua kama ana furaha bila wewe!
  • Mahusiano mara nyingi husababisha kugawana pesa na rasilimali, kwa hivyo kagua matumizi yako na ufanye marekebisho ikiwa ni lazima.