'Jezi za mpira wa miguu imekuwa kitu cha anasa'

Kombe la Dunia la FIFA la 2022 la Wanaume sio tu kwamba ndilo ghali zaidi kuwahi kutokea kwa wenyeji Qatar: mashabiki ulimwenguni kote wanaotaka kununua jezi mfano wa timu zao za kitaifa wanazozipenda lakini wanalazimika kugharamika zaidi.
Katika baadhi ya nchi, hiyo inamaanisha kutumia zaidi ya theluthi moja ya kile mtu anayepata mshahara wa chini kabisa hufanya kwa mwezi.
Janine Garcia hakufikiria mara mbili alipoliona duka linalouza jezi kwenye uwanja wa Saens Pena, mahali maarufu pa kukusanyika wachuuzi wa mitaani katika upande wa kaskazini wa Rio de Janeiro.
Ilikuwa ni yenye rangi za manjano na bluu, iliyopambwa na mamia ya jezi ya timu ya taifa ya Brazili yaliyokuwa yananing’inia kila kona.
"Nilipata ya buluu (rangi ya ukanda wa pili wa Brazili). Ni maridadi sana kwamba kundi la wafanyakazi wenzangu na marafiki tayari wameniomba niwapatie pia," mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 42 anasema, huku akicheka.
Jezi hiyo ilimgharimu Garcia sawa na dola 14, ambayo ni takribani thuluthi moja tu ya bei ya sare rasmi zinazozalishwa na kampuni kubwa ya nguo ya Marekani ya Nike ($65).
Pia kuna toleo la kwanza, ambalo ni sawa na jezi ambazo wachezaji wa Brazil wanavaa kwenye Kombe la Dunia la 2022, lakini hii gharama yake ni $130.
Kwa sasa, kima cha chini cha mshahara kwa mwezi nchini Brazili ni karibu $225.
Gharama ya jezi rasmi ya bei nafuu inafikia karibu 30% ya takwimu hiyo na ghali zaidi, karibu 58%.
Kupanda kwa bei
"Jezi za mpira wa miguu zimekuwa bidhaa ya anasa kwetu," Garcia anasema.

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Katika makala ya mwezi Septemba, jarida la biashara la Brazil la Exame liliripoti kwamba toleo jipya zaidi la jezi za Brazil zilizozinduliwa kabla ya Kombe la Dunia zimepanda bei kwa asilimia 40 tangu michuano ya miaka minne iliyopita, licha ya Brazil kutofanya vizuri kwa viwango vyao - washindi mara tano wameshindwa kutinga hatua ya robo fainali kwa mara ya tatu katika majaribio manne tangu mara ya mwisho kubeba kombe hilo, mwaka 2002.
Lakini Brazil sio nchi pekee ambapo gharama ya jezi ya soka imeibua hisia na malalamiko.
Nchini Uingereza, ambayo inakabiliwa na mzozo mkubwa zaidi wa kiuchumi katika kizazi hiki, kupanda kwa bei za jezi na bidhaa zingine za Kombe la Dunia la 2022 kulifanya jezi ya sasa ya Uingereza kuwa ghali zaidi kuwahi kutolewa ($85 kwa toleo la msingi).
Ongezeko la bei la hapo awali lilikabiliwa na ukosoaji kutoka kwa wanasiasa, akiwemo Waziri Mkuu wa zamani David Cameron.
"Ni ghali sana. Wazazi wako chini ya shinikizo kubwa kununua jezi za hivi punde na hatupaswi kuchukuliwa hili kama fursa ya kuwabana zaidi wanunuzi," Cameron aliambia BBC mwaka wa 2014.
Mashabiki wa Ufaransa waliokuwa wakitafuta jezi mpya za mabingwa wa sasa wa shindano hilo walitarajiwa kutumia karibu $93.
Timu zote mbili zina Nike kama wasambazaji wa bidhaa.
Bado katika nchi hizi athari kwenye jinsi mashabiki watagharamika si juu sana ikilinganishwa na wenzao wa kimataifa: nchini Uingereza, kima cha chini cha mshahara cha kitaifa kwa saa ni karibu $11.50, ambayo inaweza kuwa sawa na takriban $1,750 kwa mwezi.
Nchini Ufaransa, kima cha chini cha mshahara kwa mwezi ni sawa na karibu $1,400.

Chanzo cha picha, Getty Images
Uwezo wa kununua jezi rasmi za timu ambazo shabiki anapenda hauko karibu na ule wa Ghana, ndiyo maana wafuasi wa nchi hiyo walijitokeza kwenye mitandao ya kijamii mapema mwaka huu kueleza kutoridhika kwao na habari kwamba jezi ya "Black Stars" ya Kombe la Dunia, iliyotengenezwa na kampuni ya nguo ya Ujerumani Puma, ilikuwa na bei ya uzinduzi karibu $94.
Je, [jezi] bandia bado haijatoka?"aliuliza mnunuzi mmoja.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Kwa sasa, kima cha chini cha mshahara kisheria katika nchi ya Afrika, kulingana na Wizara ya Ajira na Mahusiano ya Kazi, ni $0.95 kwa saa - au labda karibu $145 kwa mwezi.
Nchini Senegal, ambao ndio mabingwa wa sasa wa Afrika, mahitaji ya nguo bandia yalikuwa juu katika mitaa ya mji mkuu Dakar, licha ya ombi la shirikisho la soka la nchi hiyo kutaka mashabiki kununua jezi rasmi, ambayo pia ilitengenezwa na Puma, ili "kuunga mkono taifa ya timu".
Kufikia tarehe 14 Novemba, jezi rasmi ilikuwa unauzwa karibu dola 71, ambayo inalingana na zaidi ya 75% ya mshahara wa chini wa kila mwezi wa Senegal wa $0.52 kwa saa ($79/mwezi), kulingana na Wizara ya Kazi.
"Jezi rasmi ni ghali sana. Ni zuri, lakini watu hapa hawana pesa," Malik, mchuuzi wa mitaani wa Senegal aliiambia Radio France International.
"Ninazidi kupata wateja zaidi na zaidi," mchuuzi alisema, kabla ya kueleza matumaini yake kwamba timu ya Senegal itafuzu kwa hatua ya muondoano, kwani hii itamruhusu kuongeza bei ya jezi.
Uchumi wa jezi
Jezi ya mpira wa miguu sio bidhaa ya bei ghali kutengeneza.
Richard Denton, mhadhiri katika Taasisi ya usimamizi wa michezo ya Johan Cruyff ya Barcelona, anakadiria kuwa ziligharimu chini ya $10 kwa kitengo kuzalisha.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Bila shaka hufanya bei ya mwisho kuonekana juu sana na mtu anaweza kusema kwamba hakuna uhalali kwa hilo," Denton anasema.
"Lakini ni bei gani isiyofaa kwa mtu mmoja inaweza kuwa nzuri kwa mwingine, kwani kuna gharama zingine na uwekezaji unaohusika ambao huathiri bei ya mwisho."
Mwanauchumi Cesar Grafietti, ambaye ni mtaalamu wa biashara ya soka, anaeleza kuwa bei ya mwisho ya jezi ya mpira wa miguu haifafanuliwa kimsingi na gharama za uzalishaji - ni kodi na gharama za vifaa ikiwa ni pamoja na usafiri ambayo ina athari kubwa zaidi.
Haya yameongezeka tangu janga la virusi vya corona, ambalo limezuia usambazaji, na vita vya Ukraine, ambavyo vimeongeza gharama za mafuta ulimwenguni.
"Makampuni ya nguo kwa kweli hayatengenezi kiasi kikubwa cha pesa kutokana na mauzo ya jezi, kwani pia wanapaswa kulipa vilabu vya juu na mashirikisho ya soka ya kitaifa malipo ya juu ili kupata haki ya kutengeneza jezi zao," Grafietti anaongeza.
Ushindani wa kampuni kubwa kubwa
Kupata fursa hii kwa makampuni makubwa kama vile Nike na wapinzani wa Ujerumani Adidas hutumia gharama kubwa kuhakikisha timu zenye hadhi kubwa zinavaa nguo hizo.
Katika michuano ya sasa ya Kombe la Dunia, Nike ndio wasambazaji wa timu 13 kati ya 32 zinazoshiriki, huku Adidas wakiwa na timu saba, wakiwemo mabingwa mara nne Ujerumani, mabingwa mara mbili Argentina na kipenzi kingine cha michuano hiyo, Uhispania.
Watengenezaji hawa wakuu kwa pamoja hutoa vifaa vya kampuni kubwa za michezo - Argentina, Brazili, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Italia na Uhispania - na hulipa mashirikisho yao ya kitaifa $275 kwa mwaka mzima kwa fursa hiyo, kulingana na tovuti ya biashara ya michezo SportsPro Media.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kampuni hizi zina wanahisani ambao hakika hawatapenda ikiwa Adidas au Nike hawatarejesha uwekezaji huo katika mikataba na timu za kandanda," Denton adokeza.
"Lakini lazima tuamue wenyewe kama jezi ni ghali au la. Ndiyo maana baadhi ya watu wanakunywa mvinyo za bei nafuu na wengine wanakunywa za bei ghali."
BBC iliwasiliana na Adidas, Puma na Nike kwa maoni.
Ingawa hadi wakati wa kuandika taarifa hii, ni Adidas pekee ndio ilikuwa imejibu.
Katika taarifa, kampuni hiyo ilisema kuwa bei ya mwisho inaonyesha ubora wa kitambaa kinachotumiwa kwenye jezi na uendelevu wake.
"Jezi zetu zina ubunifu wa vitambaa sawa na zile zinazovaliwa uwanjani na zimeundwa na kuzalishwa ili kuvaliwa kwa fahari na mashabiki kwa miaka mingi ijayo. Bei hiyo inaakisi kiwango cha uendelevu na uvumbuzi wa utendakazi unaozifanya kuwa hai."
Kwa kuuzwa kama kitu adimu Janine Garcia na marafiki zake wanajiepusha na jezi rasmi, lakini si kila mtu anaonekana kusikitishwa na bei ya juu: katika makala ya jarida la Exame iliyoripoti kupanda kwa bei ya 40% ya jezi ya Brazil, wawakilishi wa Nike walisema kuwa jezi za mwaka huu za Qatar ndizo zilizouzwa zaidi katika miaka 26 ya ushirikiano kati ya kampuni hiyo na shirikisho la soka la Brazil (CBF).
Lakini Garcia hakubaliano na hilo pia.
"Ningependa kujua ni nani anayezinunua, kwani najua watu wengi wenye pesa waliishia kununua zile za bandia ili kupata faida nzuri," anasema.
"Sio kama ni vazi ambalo utavaa kila wakati."















