Kombe la Dunia Qatar 2022: Hervé Renard, kocha wa Saudia aliyetoka kuzoa taka hadi kuifunga Argentina ya Messi

Chanzo cha picha, Getty Images
Ushindi wa Saudi Arabia wa mabao 2-1 dhidi ya Argentina umewaacha mashabiki wa kandanda vinywa wazi na sababu nzuri tu.
Miaka 4 tu iliyopita, katika mechi yao ya kwanza kwenye Kombe la Dunia la 2018 nchini Urusi, wale wanaoitwa "Green Hawks" walipoteza 5-0 dhidi ya wenyeji na wakatolewa katika raundi ya kwanza.
Kwa historia hii, haishangazi kwamba hakuna mtu aliyefikiria kikosi kinachoongozwa na Lionel Messi kinaweza kushindwa.
Walakini, zaidi ya makosa yaliyofanywa na timu inayoongozwa na Messi, au kwa bahati mbaya, tayari kuna wale ambao wamemgundua mtu aliyehusika katika kuitia aibu timu hiyo. Naye si mwengine bali kocha wa timu ya taifa ya Saudia, raia wa Kifaransa Hervé Renard.
Renard, 54, alijaribu kufanya kazi kama mchezaji wa kulipwa. Akiwa na umri wa miaka 15 alifanyiwa mtihani na Cannes, lakini ndoto hiyo iliisha haraka jinsi ilivyoanzishwa.
"Nilipokabiliana na wachezaji wengine niligundua kuwa sikuwa mzuri," alikiri katika mahojiano na Reuters miaka 4 iliyopita.
Walakini, hakukata tamaa na aliendelea kucheza ingawa hakuwahi katika vilabu vikubwa. Akikaribia umri wa miaka 30 na baada ya kuishia katika timu za "kiwango cha tatu", Renard aliacha tacos na kujitolea kukusanya na kufanya usafi.
"Mara nyingi nakumbuka miaka hiyo nilipoamka saa 3 asubuhi kwenda katika kusafisha majengo . Hunisaidia kuweka haya yote katika mtazamo mzuri," aliambia shirika la habari la Uingereza.
Pia amekiri kwamba asili yake ya unyenyekevu imemruhusu kukabiliana na shinikizo kwa njia tofauti na takwimu nyingine za soka.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kama hachezi.. anafanya mazoezi
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Licha ya ukweli kwamba ilionekana kuwa ameacha mpira, haikuwa hivyo. Kwa hivyo Renard alianza kufundisha timu za wachezaji chipukizi . Hii ilifungua milango yake kuwa mkufunzi alipopewa jukumu la kuiongoza timu ya Ufaransa ya SC Draguignan SC 1999.
Baada ya kuisaidia klabu hii kupanda daraja, Renard alipokea kutoka kwa mtani wake Claude Le Roy ofa ya kuwa naibu wake katika klabu ya Shanghai Cosco ya China ambako alikaa msimu mmoja kabla ya kuinoa Cambridge United ya Uingereza, iliyokuwa ligi ya daraja la tatu.
Aliondoka Visiwa vya Uingereza kusimamia Nam Dinh ya Vietnam na kisha akarejea Ufaransa, ambapo kati ya 2005 na 2007 aliifunza klabu ya AS Cherbourg.
lakini, alianza kujijengea umaarufu na timu za Kiafrika. Akiwa na timu ya taifa ya Zambia alishinda Kombe la Mataifa ya Afrika 2012, kombe ambalo alilipata tena 2015 akiwa na Ivory Coast.
Mnamo 2016 alikubali kuifundisha Morocco, ambayo mwaka mmoja baadaye ilifanikiwa kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2018 nchini Urusi, ikiwa ni mara ya kwanza katika miongo miwili kwa timu ya nchi hiyo ya Maghrebi kufanikiwa.
Tangu 2019 ameiongoza timu ya Saudi Arabia, ambayo ameisaidia kupanda nafasi 20 katika orodha ya FIFA duniani.
Yeye ni zaidi ya shati lake jeupe
Renard amekuwa maarufu kwa kwenda kwenye mechi akiwa amevalia shati jeupe la mikono mirefu. Katika mahojiano naye miezi kadhaa iliyopita alikiri kwamba anafanya hivyo sio kwasababu ya kuamini ushirikina.
"(Katika mechi na Zambia) nilivaa shati la bluu tukapoteza, kwa hivyo katika mechi iliyofuata nilivaa nyeupe na tukashinda," alisema.
Hata hivyo, zaidi ya mavazi yake, aina yake ya ufundishaji inayotokana na kumiliki mpira na presha kubwa ya kuuokoa, pamoja na kutilia mkazo hali ya kimwili ya wachezaji, pia ameanza kutambuliwa na wataalamu katika uwanja wa soka.
"Moja ya kumbukumbu nilizonazo kuhusu kocha Hervé ni kasi ya kazi yake, mahitaji yake kwetu sisi uwanjani na kwenye mazoezi. Maandalizi ya msimu pamoja naye yalikuwa na yanaendelea kuwa magumu zaidi kuwahi kuyafanya," John Ruddy, ambaye alichezea Cambridge United wakati kocha huyo alipokuwa mkufunzi wa klabu hiyo aliambia gazeti la the Guardian.
"Hervé angetuweka kwenye gym kufanya push-ups kwa dakika 2. Nakumbuka alikuwa akitetemeka kama mbwa na alichokifanya ni kucheka na kupiga kelele: 'John!'" aliniita, akiongeza: "Alikuwa akipiga sit Ups yeye mwenyewe kwa dakika 5 na alikuwa na umbo zuri ."















