Kwanini shambulio la ndege isiyo na rubani dhidi ya Kremlin ni la aibu sana kwa Urusi

.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Anga ya Kremlin inatakiwa kuwa chini ya ulinzi mkali

Taarifa ya kushangaza kutoka kwa utawala wa rais wa Urusi ilidai kuwa Ukraine imetumia ndege mbili zisizo na rubani kushambulia Kremlin - katikati mwa Moscow - usiku kucha.

Vikosi vya Urusi inaonekana vilitumia vifaa vya rada kuzima drones. Hakukuwa na majeruhi, na rais hakujeruhiwa, ilisema.

Lakini Kremlin ililitaja"jaribio hilo kuwa la mauaji" dhidi ya Vladimir Putin.

Kisha video kadhaa ziliibuka, zikionyesha angalau ndege moja isiyo na rubani ikiruka kuelekea Kremlin, ikifuatiwa na mlipuko. Nyingine inaonekana kuonyesha moshi ukifuka kutoka kwa jumba la Kremlin, na moto. BBC imeshindwa kuthibitisha kuwa ilikuwa ndege isiyo na rubani na haijulikani ni nini hasa kilitokea.

Lakini ikiwa kile Kremlin inachosema ni kweli, na hili lilikuwa jaribio la kweli kwa maisha ya rais, basi litakuwa tukio la aibu sana kwa Kremlin.

Kwa maelezo yote, Bw Putin anaonekana kuwa mmoja wa viongozi wanaolindwa kwa karibu zaidi duniani. Katika hafla zake huko Moscow zilizohudhuriwa na waandishi wa habari wa BBC, ulinzi mkali umekuwa ukiwekwa, pamoja na ukaguzi wa kina na msafara mrefu wa magari, huku anga ikifungwa na trafiki kusimamishwa.

Maswali sasa yataulizwa kuhusu jinsi kiongozi wa Urusi anavyolindwa - na kuhusu ufanisi wa ulinzi wa anga ya Urusi.

Katika miezi ya hivi karibuni, mifumo ya kuzuia ndege imeonekana kwenye paa za Moscow karibu na majengo muhimu, kiwemo wizara ya ulinzi. Imewekwa hapo haswa kwa sababu hii - kwa sababu Kremlin ina wasiwasi kwamba Ukraine, au wale wanaoiunga mkono Ukraine, wanaweza kujaribu kufanya mashambulio katika maeneo yenye umuhimu mkubwa.

Kulingana na shambulio hilo la drni niwazi kwamba mikakati iliowekwa ilifeli

.
Maelezo ya picha, Kremlin
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Hili ni shambulio la hivi punde zaidi katika msururu wa mashambulio na milipuko ambayo imepiga eneo la Urusi katika wiki na miezi ya hivi karibuni.

Siku chache zilizopita kumekuwa na ongezeko la matukio kama haya. Siku ya Jumatano asubuhi, ghala la mafuta lilishika moto katika Mkoa wa Krasnodar nchini Urusi, unaoripotiwa kusababishwa na shambulio la ndege isiyo na rubani.

Treni mbili za mizigo ziliacha njia katika Mkoa wa Bryansk, karibu na mpaka na Ukraine, Jumatatu na Jumanne, katika matukio tofauti lakini yanayofanana. Gavana wa eneo hilo alisema vilipuzi ndivyo vilivyosababisha hali hiyo.

Mwishoni mwa juma, maafisa waliowekwa na Urusi katika eneo linalokaliwa la Crimea walidai ndege zisizo na rubani za Ukraine zilihusika na shambulio kwenye kituo cha kuhifadhi mafuta.

Mashambulizi kama hayo husababisha woga kati ya raia wa Urusi.

Vyombo vya habari vya Urusi vinaripoti kwamba polisi huko Moscow wamekuwa wakipokea simu kutoka kwa umma wakiripoti kuonekana kwa ndege zisizo na rubani katika mji mkuu.

Ukraine imekanusha vikali kushambulia Kremlin au kumlenga Rais Putin. Lakini ikiwa madai yanayotolewa ni ya kweli au la, swali ni iwapo Urusi italipiza kisasi na iwapo itafanya hivyo itatumia mbinu gani.

Baadhi ya maafisa wa Urusi tayari wametaka hatua kali zichukuliwe. Jaribio la mauaji dhidi ya rais, ikiwa ndivyo ilivyokuwa, ni jambo zito sana. Majenerali wa Urusi wameonya mara nyingi juu ya majibu makali dhidi ya mashambulizi ndani ya Urusi.

Lakini je, Urusi ina uwezo wa kutekeleza mashambulizi yoyote ya kuliupza kisasi? Inasalia kuonekana ikiwa tukio hili litasababisha ongezeko lolote kubwa la kivita