Bayraktar TB2 ya Uturuki: Kwa nini mataifa ya Afrika yananunua silaha hii hatari?

Chanzo cha picha, Getty Images
Mataifa mengi ya Afrika yanazidi kununua ndege za kivita zisizo na rubani za Uturuki ili kupambana na makundi yenye silaha baada ya kuthibitisha kuwa zina ufanisi katika migogoro mbalimbali duniani, kulingana na mchambuzi Paul Melly.
Wakati Ukraine ilipoimarisha vita dhidi ya uvamizi wa Urusi nchini humo , na kabla ya kupokea silaha nzito nzito kutoka kwa washirika wake wa Magharibi , kulikuwa na silaha moja ambayo serikali ya Kyiv ilikuwa ikiitumia – nayo ni ndege isiyo na rubani ya Bayraktar TB2.
Silaha hii iliyotengenezwa nchini Uturuki tayari ilikuwa imethibitisha ufanisi wake baada ya kuisaidia Azerbaijan kulishinda jeshi la Armenia na kukomboa eneo kubwa la vita vya Nagorno-Karabakh 2020.
Lakini wanaovutiwa na silaha hii hawako Ulaya Mashariki na Caucasus pekee.
Wiki za hivi karibuni zimeshuhudia shehena ya Bayraktar TB2 ikipelekwa katika bara la Afrika hususani Magharibi mwa Togo, ambapo taifa hilo linajitahidi kuwazuia wapiganaji wa kijihadi kutohamia katika taifa hilo kutoka Burkina Faso.
Mwezi Mei, Niger ilipata nusu dazeni ya ndege hizi zisizo na rubani zinazoweza kutumika kwa wingi kwa bei nafuu kwa ajili ya operesheni zake za kijeshi dhidi ya makundi ya waasi katika eneo la Sahel kusini mwa Jangwa la Sahara, na karibu na Ziwa Chad.
Wateja wengine wa bara Afrika wamejumuisha Ethiopia, Morocco na Tunisia, wakati Angola pia ikiwa na nia ya kununua.
Lakini ya kwanza kutumia silaha hizi zenye nguvu za uchunguzi na kushambulia katika bara hilo inaweza kuwa serikali inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa nchini Libya – ambapo zilionekana mapema mwaka 2019 na kusaidia vikosi vya Tripoli kuwazuia waasi wa mashariki.
Kwa wanunuzi wa Afrika, hasa nchi maskini zaidi, ndege zisizo na rubani hutoa fursa ya kuwa na silaha yenye uwezo mkubwa angani bila gharama kubwa ya vifaa na mafunzo ya miaka mingi yanayohitajika ili kuunda kikosi cha kawaida cha mashambulio ya ndege za kivita angani .
Hiki ni kivutio mahususi kwa mataifa kama vile Niger na Togo.
Wanakabiliwa na changamoto tata ya kuzuia vikundi vya wapiganaji wa Kiislamu wenye ari kubwa na wanaohamahama, kupiga kambi msituni na kusonga kwa haraka katika eneo lenye la Sahel kwa pikipiki ili kufanya mashambulio ya kuvizia na mashambulizi ya kushtukiza kwenye vituo vilivyotengwa vya jeshi, kuvuka mpaka na kushambulia.

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Jeshi la Niger limekuwa likikabiliana na tatizo hili kwa miaka mingi, likipambana na wanamgambo katika eneo la mpakani, ambapo nchi hiyo inapakana na Burkina Faso na Mali, umbali wa saa chache tu kwa gari kutoka mji mkuu, Niamey.
Wanajeshi wa serikali pia wanashiriki katika kampeni kali ya kulinda eneo la kusini-mashariki kutokana na mashambulizi ya Boko Haram pamoja na yale kutoka kwa na wapiganaji wa Kiislamu wa Jimbo la Afrika Magharibi (Iswap).
Lakini kwa Togo, ukweli wa moja kwa moja wa tishio la wanajihadi ni uzoefu mpya na unaotia wasiwasi sana.
Kwa muda mrefu wa muongo mmoja uliopita shughuli za vikundi vya wanamgambo zilijikita katika eneo la kati la Sahel - Mali, Burkina Faso na Niger - na hasa katika maeneo ya mbali na mipaka yao na nchi za pwani kama vile Ivory Coast, Ghana, Togo na Benin.
Lakini hivi majuzi taswira imeanza kubadilika, kwani vikundi vilivyojihami vilipanua ufikiaji wao katika sehemu kubwa ya Burkina Faso, na katika maeneo ya vijijini kwenye mpaka na hizi nne .
Kufikia mwishoni mwa 2019 vikosi vya usalama vilikuwa vikigundua dalili za kupenya kwa wanamgambo kaskazini mwa Togo.
Hapo awali wapiganaji walikuwa wamejificha kwa ajili ya kupumzika na , lakini serikali ya Lomé, kama wenzao katika pwani ya Afrika Magharibi, tayari ilikuwa na wasiwasi kwamba tishio hilo lingeweza kuongezeka.
Nchi jirani ya Ivory Coast ilikumbwa na shambulio la wanajihadi kwenye eneo la mapumziko la Grand Bassam mwaka 2016, ambalo lilisababisha vifo vya watu 19, kisha mashambulizi na mapigano na vikosi vya usalama kaskazini-mashariki mwaka 2020.

Chanzo cha picha, Getty Images
Na afisa anayeongoza safari za kuwatazama wanyamapori aliuawa wakati wapiganaji walipowateka watalii wawili wa Ufaransa katika mbuga ya wanyamapori ya Penjari nchini Benini.wanajeshi hao wa Ufaransa baadaye waliuawa katika ufyatulianaji wa risasi wakati watalii hao walipookolewa ndani ya mpaka wa Burkina Faso.
Uvamizi wa kwanza wa moja kwa moja dhidi ya Togo katika Eneo la Sanloanga, ulifanyika mwezi Novemba. Kabla ya alkfajiri ya tarehe 11 mwezi Mei , makumi ya wapiganaji walishambulia kituo kimoja cha jeshi karibu na taifa la Burkina Fasso , na kuwauawa wanajeshi wanane na kuwajeruhi wengine 13.
Wanajeshi hao walifanya mashambulizi na kuwauawa baadhi ya wapiganaji . Mwezi uliofuata iliweka hali ya tahadhari katika eneo la Savanes, jimbo la kaskazini mwa Togo.
Lakini hilo halijatosha kuwazuia wanajihad wanaofanya operesheni zao katika mstari wa mbele na wanaodaiwa kushirikiana na kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Jama'a Nusrat ul-Islam wa al-Muslimin, Mjuungano mkubwa wa wapiganaji wa Kiislamu kutoka Mali .wanajeshi wengine wawili waliuawa katika tukio jingine mwezi Julai.
Rais Faure Gnassingbe, ametembelea eneo hilo katika juhudi kuwapatia motisha raia wake. Lakini Baadhi ya wakaazi walio na hofu wamekuwa wakitoroka vijiji vyao -tatizo ambalo tayari limeanza kuonekana katika maeneo mengine yalioathiriwa na ghasia za wapiganaji.
Utawala huo ambao umechukua mdaraka kwa miongo kadhaa pia umeona umuhimu wa kuvialika vyama vya upinzani kwa mazungumzo ya kuungana dhidi ya tishio la wapiganaji hao.
Lakini mwishowe, nguvu ya kijeshi ya moja kwa moja italazimika kutumika. Na hapo ndipo ndege zisizo na rubani za Uturuki zinapokuja, zikiipa Togo - kama Niger - uwezo wake wa kitaifa wa uchunguzi wa angani kujaribu kuona vikundi vya wapiganaji na ikiwezekana, kuvishambulia.
Utumiaji wa ndege zisizo na rubani sio jambo geni kwa eneo la Sahel. Ufaransa na Marekani zina kambi za ndege zisizo na rubani nchini Niger, zinazofanya kazi kuunga mkono mkakati wa usalama wa serikali.
Kwa mataifa makubwa kama vile Ethiopia - ambapo serikali ya shirikisho imekuwa ikipambana na wapiganaji wa Tigray People's Liberation Front - ndege zisizo na rubani ni chombo muhimu cha kupanua uwezo wa kijeshi kwa ujumla.
Lakini kuna hatari, kama ilivyo kwa ndege za kivita zenye rubani. Kufikia Januari, wafanyakazi wa misaada walikuwa wakiripoti kwamba ndege zisizo na rubani zimeua zaidi ya raia 300 katika mzozo wa Tigray nchini Ethiopia.
Na jeshi la Togo limekiri kuwaua raia saba vijana kimakosa, baada ya ndege ya kivita - iwe ya mtu au isiyo na rubani haijulikani - kudhania walikuwa kundi la wanamgambo na walianzisha mashambulkizi Julai 9-10.
Hatari za makosa hayo ya kusikitisha huongezeka wakati wa hofu juu ya kujipenyeza kwa wanajihadi.
Kwa Togo na Niger ushirikiano wa ununuzi wa silaha hiyo kutoka kwa Uturuki pia ni muhimu kisiasa, kwasababu unapunguza utegemezi wao wa usalama wa umma kutoka kwa Ufaransa, koloni la zamani, ambalo raia wengi hawana imani nalo.
Kwa mtazamo wa Ankara pia kuna vivutio: "diplomasia ya ndege zisizo na rubani" na ushirikiano wa kijeshi umekuwa nyenzo muhimu katika sera ya nje ya Rais Recep Tayyip Erdogan kusini mwa Sahara, inayosaidia nguvu zaidi za muda mrefu kama vile ujenzi wa viwanja vya ndege na mambo mengine muhimu kama miundombinu.
Baykar, kampuni inayotengeneza ndege isiyo na rubani ya Bayraktar TB2,inaongozwa na ndugu wawili – Afisa Mtendaji Mkuu Haluk Bayraktar na kaka yake Selçuk, Afisa Mkuu wa Teknolojia, ambaye amemuoa binti wa Rais Erdogan Sümeyye.












