Zijue faida za tango kwa wanawake

Chanzo cha picha, Getty Images
Kulingana na Dk Prachi Garg akieleza katika mtandao wa PhramaEasy, unywaji wa juisi ya tango hupunguza hatari ya saratani kwa wanawake hasa saratani ya shingo ya kizazi na saratani ya mapafu. Tango huzuia magonjwa mengi na hupambana na unene.
Tango lina faida nyingi kiafya, limejaa vitamini K, C, na A, pia zinapatikana nyuzinyuzi na madini ya potasiamu na kalisi (calcium). 95% ya tango ni maji hivyo huulinda mwili kutokana na ukavu.
Faida nyingine za tango

Chanzo cha picha, Getty Images
Hupunguza maumivu kwenye viungo na mifupa: Osteoporosis ni ugonjwa wa mifupa, husababisha mifupa kuwa dhaifu na unaweza kusababisha mifupa membamba kuvunjika hata ikiwa umepinda kidogo. Matango yana madini kama kalsiamu, shaba, magnesiamu na potasiamu ambayo huimarisha afya ya mifupa na matatizo ya mifupa yanayohusiana na umri.
Huzuia saratani: Matango huzuia baadhi ya aina za saratani kama vile saratani ya tezi dume. Kulingana na Jarida la utafiti wa mitindo na maisha la Edging.
Hupunguza uzito: Tango husaidia sana kupunguza uzito, linaweza kumsaidia mtu kupungua kwa kupata virutubisho vingi muhimu.
Tango lina nafasi kubwa katika urembo: wa nywele, ngozi na kucha.

Chanzo cha picha, Getty Images
Matango huimarisha afya ya akili: Matango yana flavonoids, ambayo ina nguvu ya kuboresha afya ya akili. Inaboresha kazi ya ubongo na huongeza kumbukumbu. Pia hulinda seli kutokana na uharibifu unaohusiana na kuzeeka.
Watafiti wanasema tunda hili huboresha kinga ya mwili.
Ni tiba ya bawasiri: Tango hutuliza bawasiri na huondoa maumivu.
Hufanya kazi muhimu katika usagaji chakula: Tango lina nyuzinyuzi nyingi na maji, ambavyo vyote ni muhimu kwa usagaji chakula. Vilevile huzuia kiungulia. Kunywa juisi ya tango kila siku husaidia kutibu vidonda vya tumbo.
Miongoni mwa faida zilizotajwa na watafiti za tango ni kupunguza kuzagaa kwa chembechembe zisizo za kawaida mfano za saratani.
Pia, lina uwezo wa kupambana na bakteria, fangasi na virusi, na baadhi ya watafiti wanapendekeza watu wanaotumia dawa za VVU kula tango - ili kupunguza virusi kuzaliana.












