Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa: Je, Tottenham kumrejesha Palhinha EPL?
Tottenham inajadiliana na klabu ya Bayern Munich kuhusu uwezekano wa kumsajili kwa mkopo wa mchezaji wa kimataifa wa Ureno Joao Palhinha, 30, huku ikitarajia kumrejesha kiungo huyo wa zamani wa Fulham kwenye Ligi ya Premia. (Athletic - usajili unahitajika)
RB Leipzig ni miongoni mwa vilabu kadhaa vinavyomfuatilia Rasmus Hojlund na Manchester United huenda ikamtumia mshambuliaji huyo wa Denmark mwenye umri wa miaka 22 kama sehemu ya makubaliano ya mkataba wa kumsajili mshambuliaji wa Slovenia Benjamin Sesko, 22. (Athletic - usajili unahitajika)
Mchezaji wa Manchester United Jadon Sancho, 25, yuko tayari kukatwa 50% ya mshahara wake ili kuondoka klabu hiyo na anapania kurejea katika klabu ya Bundesliga ya Borussia Dortmund. (Bild - kwa Kijerumani)
Chelsea inatarajiwa kuwasilisha ombi la kumsajili mchezajili mchezaji wa Manchester United Alejandro Garnacho, 21, kabla ya dirisha la usajili kufungwa na haina wasiwasi wowote kuhusu tabia yake baada ya kumchunguza winga huyo wa Argentina. (Telegraph - usajili unahitajika)
Kiungo wa England Nico O'Reilly, 20, atatia saini mkataba mpya na Manchester City baada ya kukataa ofa mbili za uhamisho kutoka kwa klabu ya Ujerumani Bayer Leverkusen. (Fabrizio Romano)
Klabu ya La Liga Girona imefikia makubaliano ya kimsingi ya kumsaini beki wa Manchester City Mbrazil Vitor Reis, 19, kwa mkopo. (Fabrizio Romano)
Manchester City pia inamtaka Claudio Echeverri, 19, kujiunga na klabu ya Girona kwa mkop wa msimu mzima, huku majadiliano yakiendelea kati ya winga huyo wa Argentina na klabu hiyo ya Uhispania. (Fabrizio Romano)
Chelsea inavutiwa na Ardon Jashari wa Club Brugge lakini kiungo huyo wa Uswizi mwenye umri wa miaka 23 anapendelea kuhamia AC Milan. (Sacha Tavolieri)
Everton itasubiri hadi wiki za mwisho za msimu wa uhamisho wa wachezaji ili kuwasilisha ofa ya kumsajili kwa kiungo wa Juventus na Brazil Douglas Luiz, 27. (GiveMesport).
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi