Je, Wamarekani Waarabu watamuangusha Rais wa Marekani Donald Trump?

Muda wa kusoma: Dakika 5

Wamarekani Waarabu na Waislamu walishiriki katika kumrejesha Donald Trump Ikulu ya White House.

Ingawa asilimia yao nchini Marekani si kubwa, ushawishi wao ulikuwa mkubwa kwa sababu kuu mbili: ya kwanza ni mkusanyiko wao katika baadhi ya majimbo muhimu ambapo ushindani wa uchaguzi wa urais ulikuwa mkubwa, kama vile Michigan, na ya pili ni ukubwa wa ushawishi wa vyombo vya habari unaofurahia masuala yanayohusiana na Waarabu na Waislamu, hasa suala la Palestina na udhihirisho wake wa hivi karibuni katika vita vya Gaza.

Suala la kwanza bila shaka lilikuwa muhimu kwa Trump katika uchaguzi, huku la pili likiendelea kuwa muhimu huku urais wake unapoanza.

Wamarekani Waarabu na Waislamu walishangazwa kusikia mawazo ya Rais Trump mapema katika kipindi chake cha urais, ambayo yalijumuisha uhamisho wa Wapalestina kutoka Ukanda wa Gaza huku Marekani ikiashiria kutaka kulichukua eneo hilo.

Huko Dearborn, Michigan, ambako wakazi wengi ni Waarabu, jiji hilo limekuwa kielelezo wazi cha ukuu wa Trump na kuwafikia wapiga kura Wamarekani, kushinda kura zao kwa gharama ya mpinzani wake wa chama cha Democratic Kamala Harris, Makamu wa Rais wa zamani Joe Biden.

Biden alikuwa ameshinda zaidi ya theluthi mbili ya kura za wapiga kura wa Dearborn alipomshinda Trump mnamo 2020, lakini mambo yamebadilika sana miaka minne baadaye.

Pia unaweza kusoma

Niliposafiri na timu ya BBC hadi Dearborn na miji mingine ya Michigan nikiwa na habari za kampeni ya uchaguzi wa 2024, wakaazi wa Kiarabu walikasirishwa na utawala wa Biden-Harris, wakiulaumu na kuwajibika kwa vita vya Gaza na kuendelea kwake.

Miongoni mwao alikuwa Samra Luqman, mwanaharakati ambaye alikuwa Democrat na chama cha Biden lakini aliamua kumpigia kura Trump wa Republican kwa sababu alimlaumu Biden kwa kuhusika na vita vya Gaza na kushindwa kwake kuizuia Israel, alisema.

Aliniambia siku hiyo jinsi alivyoathiriwa na kuumizwa na vita vya Gaza, na pia aliniambia kuhusu mkutano wa moja kwa moja na Trump kupitia kampeni yake ya uchaguzi, ambayo aliwasiliana naye, licha ya kuwa alikuwa wa chama pinzani. Trump, alisema, alichukua hatua ya kuzungumza naye na kumwambia juu ya hitaji la kusitisha vita, na hiyo ilichukua jukumu kubwa katika uamuzi wake wa kumpigia kura.

Ingawa Trump hakuwahi kuficha kuiunga mkono Israel, hata alipokuwa rais katika muhula wake wa kwanza wala wakati wa kampeni za uchaguzi, harakati zake kuwarai Waamerika Waarabu kumuunga mkono zilifanikiwa, kwani alizingatia wazo la ahadi yake ya kumaliza vita Mashariki ya Kati, na kwa madai kwamba vita hivyo havingezuka iwapo angekuwa rais.

Katika mazoezi, Trump aliitembelea Michigan mara kwa mara, na hata akaenda Dearborn yenyewe, ambapo wapiga kura wa Kiarabu walimsherehekea na kujibu ahadi zake za kumaliza vita na kuanza enzi mpya.

Mwishowe, Harris alipata pigo la kisiasa alipopata asilimia 37 pekee ya kura za wapiga kura wa Dearborn, huku Trump akipata asilimia 43 ya kura zao, na kura zilizosalia zikaenda kwa wagombea wengine.

Samra alizungumza nasi sasa na kumuuliza ikiwa anajuta kumpigia kura Trump. Alisema mara nyingi hupata maswali kama, "Je, una furaha sasa kwamba Trump anatoa wito wa utakaso wa kikabila huko Gaza?" Lakini anajibu kwa dharau na ukumbusho wa kile kilichokuwa kikitokea Gaza wakati wa vita.

Samra anasema anaamini kabisa kuwa Biden asingesimamisha vita, wakati Trump aliweza kuvizuia, na kwamba matukio ya Wagaza wakirejea makwao licha ya hali zao ngumu yasingetokea ikiwa utawala wa Biden-Harris ungekuwa madarakani.

Samra anaendelea kueleza msimamo wake kwa kusema kwamba hafurahishwi na kauli za Trump kuhusu Gaza, lakini anapolinganisha jambo hilo na kile ambacho kingeweza kutokea na kuendelea kama asingesimamisha vita, hii inamfanya kuridhika, au angalau kuwa katika hali nzuri zaidi kuliko alivyokuwa wakati wa vita.

Kuhusu Bishara Bahbah, anayeongoza shirika kwa jina "Wamarekani wa Trump," na asili ya shughuli zake ni wazi kutoka kwa jina hilo: uhamasishaji wa uchaguzi na kisiasa kwa Trump. Hata hivyo, shirika hilo liliamua kubadili jina lake kuwa "Wamarekani wa Amani."

Bahbah anaeleza kuwa mabadiliko ya jina yalikuja na kauli za Trump kuhusu kuwahamisha Wapalestina kutoka Gaza nje ya Ukanda huo na kuuteka Ukanda huo, lakini anasema kuwa sababu ya moja kwa moja ya mabadiliko hayo ni kwamba awamu mpya imeanza katika uhusiano wa shirika lake na Waamerika wa Kiarabu na Trump, ambayo ni kwamba amekuwa rais na kwamba uchaguzi wa rais umeamuliwa.

Mawazo hayo ya Trump yaliwashangaza wapinzani wake wa kisiasa nchini Marekani, ambao walimkosoa vikali. Kwa mfano, Seneta Tim Kaine, anayewakilisha jimbo la Virginia, ambalo lina wapiga kura wengi wa Kiarabu na Waislamu, na ni kiongozi wa Chama cha Democrats cha Biden, ambaye alielezea mawazo ya Trump kama "kichaa." Mwakilishi pekee wa Marekani mwenye asili ya Palestina, Rashida Tlaib wa Michigan, alimshambulia vikali Trump na kauli zake.

Huko Dearborn, Michigan, na maeneo mengine ya Waarabu na Wamarekani, wengi wana shaka kwamba mawazo ya Trump juu ya Gaza yatatokea, na wengi wanasema kuchaguliwa kwake kama rais angalau kumesimamisha vita na kufungua mlango wa matumaini ya ushawishi mkubwa wa Waarabu juu ya sera zake katika siku zijazo.

Bishara Bahbah anasema anataka kumkumbusha Trump kwamba kuna uchaguzi ujao wa bunge, ambapo Chama cha Republican cha Trump kina wabunge wengi katika mabunge yote mawili, Baraza la Wawakilishi na Seneti.

Uchaguzi huo utafanyika mwishoni mwa mwaka ujao, na Bahbah anaeleza: "Trump atahitaji kura zetu ili chama chake kiendelee kudhibiti mabunge yote mawili ya Congress. Tupo hapa na bado hatujamaliza.

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Seif Abdalla