Nini kiliamuliwa wakati mzozo kuhusu umiliki wa mwezi ulipozuka?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Katika miaka ya sitini , vita baridi kati ya Marekani na Usovieti viliathiri siasa duniani.

Wasiwasi uliokuwepo kati ya mataifa hayo mawili yenye nguvu Zaidi ulibadilika na kuwa ushindani katika siasa za kimataifa. Kuliwa na maeneo mawili yanayopiganiwa wakati wa vita baridi.

Kwanza ilikuwa utenegenezaji wa silaha za kinyuklia, huku mwengine ukiwa jinsi ya kuwasiliana kupitia anga ama nyota.

Vita baridi vilisababisha utafiti wa mambo mengi ya angani , na kuzua swali la ni nani anayemiliki mwezi.

Umoja wa usovieti uliishinda Marekani kwa kutua mwezini. Wakati huo uchunguzi kuhusu mwezi ulikuwa ukivutia wengi.

Usovieti ilituma setlaiti katika mwezi kati ya miaka ya hamsini na sitini . Mnamo mwezi Septemba 1959, Muungano wa Usovieti kwa sasa Urusi uliwasilisha chombo chake cha anga za mbali katika sakafu ya mwezi kwa mara ya kwanza.

Baadaye mnamo mwezi Oktoba mwaka huohuo, picha ya kwanza ilitumwa na setlaiti hiyo kutoka sakafu ya mwezi.

Halafu mwezi Februari 1966, setlaiti nyengine kwa jina Luna 9 ilizinduliwa na Usovieti ikiwa ni mara yao yan ne kufanya hivyo.

Miezi minne baadaye , Setlaiti ya Marekani kwa jina Surveyor -1 ilitua mwezini.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Mzozo kuhusu umiliki wa mwezi

"Ushindani wa utafiti wa nyota ulizua hali ya mvutano kati ya nchi za ulimwengu," mwanasayansi mkuu Vigyan Prasar Sanstha ambaye alizungumza na BBC alisema.

"Kwa sababu wakati wa ukoloni, hakukuwa na sheria iliodai kwamba kwamba nchi ya kwanza kupata ardhi mpya ni yake."

Je kandarasi ya mwezi inasema nini?

Umoja wa Mataifa umetia saini mkataba unaoitwa 'Mkataba wa Mwezi' ili kusuluhisha nani anamiliki mwezi.

Mkataba huu unasema kwamba mwezi ni mali asili ambayo ni ya wanadamu wote. Hakuna nchi inayoweza kudai mwezi au hata kuanzisha serikali juu yake.

Mkataba huu ulijadiliwa kati ya 1972 na 1979 na ulitiwa saini huko New York mnamo 1979. Lakini ulihitaji kutiwa saini na nchi tano ili uanze kutekelezwa. Ulianza kutumika mnamo 1984 wakati Austria ilipotia saini.

Lakini Marekani, Uchina na Urusi, ambazo zimetuma satelaiti mwezini, bado hazijaidhinisha makubaliano hayo.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakati wanadamu walipokwenda katika mwezi

Baada ya kupeleka mtu katika mwezi mwaka wa 1960 hadi 1970, Marekani inajaribu tena kutuma mtu mwingine kwenye sakafu ya mwezi.

Mpango unaoitwa Artemi ulianzishwa na Marekani kwa ajili ya lengo hilo.

Mpango huu unajumuisha mashirika ya Marekani ya sayansi ya anga ya juu, yale ya Canada, Japani na Ulaya. Awamu ya kwanza ya mpango huu ilianza 2022 wakati awamu ya pili inatarajiwa kuanza 2024.

Lengo la mpango huu ni kuufanya mwezi kuwa ngazi ya kuruka kuelekea sayari ya Mars.

Lakini kampuni kubwa ya NASA inataka kutumia kampuni ya sayansi ya anga inayomilikiwa na tajiri Elon Musk kupeleka binadamu katika mwezi kwa mara nyengine.

Mkataba huo ulitiwa saini na kampuni mbili za Marekani, Sech Blue na Dianetics.