Je, silaha hii ya India imeiweka miongoni mwa mataifa yenye uwezo mkubwa wa kijeshi duniani?

.

Chanzo cha picha, x.com/DRDO_India/status

Muda wa kusoma: Dakika 4

India imetangaza kuwa imefanikiwa kufanyia majaribio mfumo unaotumia teknolojia ya leza kuharibu ndege zinazoshukiwa kuwa zisizo na rubani na makombora ya adui.

Jaribio hilo lilifanywa na Shirika la Utafiti na Maendeleo la Ulinzi (DRDO) mnamo Aprili 13 katika Safu ya Kitaifa ya Anga ya Uwazi karibu na Kurnool.

India ni mojawapo ya nchi chache zilizotengeneza silaha za teknolojia ya leza, ambazo zinaitwa "teknolojia ya Star Wars" ya siku zijazo.

"Huu ni mwanzo tu wa matumizi ya teknolojia ya nguvu kupita kiasi," Mwenyekiti wa DRDO Sameer V. Kamath alitangaza baada ya kufaulu kwa jaribio hilo.

Akizungumza na BBC, mwenyekiti wa zamani wa DRDO G. Satish Reddy alisema, "Jaribio hili la India ni muhimu sana katika sekta ya ulinzi."

Pia unaweza kusoma
.

Chanzo cha picha, X.com/DRDO_ India/Status

Je, ni teknolojia ipi iliotumika?

Kadiri teknolojia inavyoendelea, mbinu za vita zinabadilika. Badala ya kutumia makombora, vita vinapiganwa kwa teknolojia ya droni.

Mashambulizi ya ndege zisizo na rubani tayari yamefanyika kwa wingi katika vita vya Ukraine na Urusi.

Imekuwa muhimu kwa kila nchi kutoa teknolojia ya kisasa ili kuzuia mashambulizi ya droni wakati wa vita vya baadaye.

Kwa hili, majaribio yanafanywa kwenye teknolojia za silaha kama vile leza yenye nguvu nyingi.

Katika muktadha huu, DRDO imetengeneza Silaha ya Nishati Inayoongozwa na teknolojia ya leza (DEW) Mk-II(A).

Satish Reddy alisema ili kukabiliana vyema na mashambulizi ya ndege zisizo na kwa sasa, ni muhimu sana kuandaa mifumo ya kuzuia silaha hizo.

Alisema kuwa silaha ya nishati inayoelekezwa kwa leza iliyojaribiwa na DRDO ina nguvu kubwa.

Silaha hiyo ya leza ilijaribiwa chini ya ufadhili wa Kituo cha Mifumo na Sayansi ya Nishati ya Juu (CHES) huko DRDO.

Ilitangaza kuwa ndege isio na rubani (UAV) lilidunguliwa kwa miale ya leza. Video inayohusiana na hii ilitolewa kwenye 'X'.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa X ujumbe

Mwenyekiti wa DRDO Sameer V. Kamath alitangaza kuwa huu ni mojawapo ya uwezo wa India wa Star Wars.

Sameer V. Kamath aliambia shirika la habari la ANI kwamba India imeorodheshwa ya nne au ya tano kati ya nchi zilizo na teknolojia ya nguvu ya juu ya leza DEW.

"Marekani, Urusi, na China wana teknolojia hii. Israel pia inaiendeleza," alisema.

DRDO imetangaza kuwa sio tu ndege nyepesi zisizo na rubani, lakini pia ndege zisizo na rubani na helikopta zinaweza kuharibiwa kabisa kwa msaada wa DEW.

.

Chanzo cha picha, X.com/DRDO_India

Maelezo ya picha, DRDO imetangaza kuwa ndege zisizo na rubani na helikopta zinaweza kudunguliwa kwa msaada wa DEW

Majaribio ya Leza kutoka 2019

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

DRDO ilitengeneza aina hii ya teknolojia ya silaha za leza mnamo 2019.

Hatahivyo wakati huo ilitumika sana kuharibu malengo ndani ya safu ya kilomita mbili.

Hivi sasa, silaha ya leza yenye uwezo wa kilowati 30 inaweza kuharibu malengo kwa umbali wa kilomita 4-5.

"Teknolojia hii ya leza inaweza kuharibu kimuundo ndege zisizo na rubani na kuzima vitambuzi vyao vya uchunguzi," DRDO ilitangaza.

Dk. W. Selvamurthy, mdhibiti mkuu wa zamani wa DRDO R&D na chansela wa Chuo Kikuu cha Amity huko Noida, aliambia BBC kuwa silaha za teknolojia ya leza zitafanya kazi mara tu ndege zisizo na zitakafika eneo maalum.

"Ndege zisizo na rubani zinapaswa kukaribia ardhi ili kushambuliwa. Pindi zinapoingia ndani ya safu maalum, zinaweza kuangushwa kwa kutumia teknolojia ya leza," alisema.

Ilielezwa kuwa athari za mihimili ya leza itakuwa chini ikiwa iko mbali.

Chuo Kikuu cha Amity kwa sasa kinafanya kazi na DRDO kuhusu teknolojia ya kupoza miale ya leza.

G. Satish Reddy alisema kuwa India ni mojawapo ya nchi ambazo zimetengeneza mfumo wa kupambana na ndege zisizo na rubani.

"Silaha za teknolojia ya leza ni muhimu sana kwa mfumo wa ulinzi wa nchi. Kwa jaribio hili, uwezo wa silaha za teknolojia ya leza umeongezeka zaidi," alisema.

.

Chanzo cha picha, X.com/DRDO_ India/Status

Maelezo ya picha, DRDO inadai kuiangusha na kuharibu ndege zisizo na rubani kwa miale ya leza

Utengenezaji wa silaha za leza zenye nguvu zaidi

DRDO kwa sasa inashughulikia utengenezaji wa silaha za leza zenye 'nguvu ya juu' zaidi. Inatengeneza silaha za leza zenye nguvu ya kilowati 300 zinazoweza kushambulia shabaha ilio umbali wa kilomita 20.

"Sasa tumeunda teknolojia ya leza ambayo inafanya kazi kutoka juu ya (ardhi). Tunaitengeneza ili itumike hewani na kwenye maji," Sameer V. Kamath aliambia shirika la habari la ANI.

Alieleza huu kuwa ni mchakato endelevu.

Kwa upande mwingine, Selvamurthy alisema kuwa suluhu zinazotegemea leza zitakuwa na gharama ya chini ikilinganishwa na makombora.

"Utengenezaji wa makombora ni jambo la gharama kubwa. Mfumo wa boriti ya leza unaweza kufanywa kwa gharama ya chini," alisema.

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Seif Abdalla