Je, wahalifu huzaliwa waovu?

Onyo - Makala haya yana maelezo ambayo baadhi ya wasomaji yanaweza kuwatatiza.
Jioni ya Agosti 20, 1989, wanandugu Erik na Lyle Menendez waliingia katika nyumba yao ya Beverly Hills, ambapo wazazi wao walikuwa wakitazama filamu ya The Spy Who Loved Me, na kuwafyatulia risasi .
Walihukumiwa kifungo cha maisha gerezani bila msamaha, na kwa miaka mingi, hadithi yao ilififia.
Kisha mnamo Septemba, hadithi yao iligonga tena vichwa vya habari baada ya mfululizo wa tamthilia ya Netflix kuangazia kile kilichowapata, na kusababisha kesi yao kuchunguzwa kwa sababu ya ushahidi mpya ambao haujawasilishwa kwenye kesi yao.
Jumatatu iliyopita, miaka 28 baada ya kufikishwa mahakamani mara ya mwisho, wanandugu walihudhuria kesi hiyo kutoka gerezani kwa njia ya simu, ambapo shangazi yao aliomba wachiwe. "Nadhani ni wakati wao wa kurudi nyumbani," alisema.
Kwa upande mwingine, mjomba wao aliwataja ndugu hao kuwa "wamwaga damu" na anaamini kuwa wanastahili kifungo cha maisha jela.

Chanzo cha picha, Getty Images
Katika miaka yangu 30 kama mtaalamu wa magonjwa ya akili anayefanya kazi katika hospitali za magonjwa ya akili na magereza kote Uingereza, ikiwa ni pamoja na Broadmoor,(hospitali maalum kusini mwa Uingereza kwa ajili ya wahalifu ambao ni wagonjwa wa akili na wanaochukuliwa kuwa hatari sana.) nimezungumza na mamia ya wahalifu ambao wametenda makosa mabaya katika kujaribu kuwajibika.
Watu wengine wanadhani kwamba hii ni kazi isiyowezekana. nimekuwa nikiulizwa: "Lakini kwa hakika haiwezekani kusaidiwa? Je, hawakuzaliwa hivyo?" Maana yake ni kwamba ni mnyama asiye wa kawaida tu ndiye anayeweza kusababisha mambo mabaya kwa mtu mwingine, au kwamba wauaji, kutoka Rose West hadi Harold Shipman, Lucy Letby hadi Peter Sutcliffe, kwa namna fulani sio wanadamu.
Hakika, nilipoanza kufanya kazi katika eneo hili, nilidhani kwamba watu ambao wamefanya vitendo vya jeuri na mauaji ni tofauti sana na sisi wengine.
Ukweli ni kuwa ni vigumu zaidi kumtaja mtu kuwa 'mwovu' tu, kama nilivyogundua moja kwa moja.
Muuaji katili 'aliye hatarini'
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Mnamo 1996, mara tu baada ya kuanza kwa Broadmoor, hospitali maalumu kusini mwa Uingereza kwa ajili ya wahalifu ambao ni wagonjwa wa akili na wanaochukuliwa kuwa hatari sana, wakati nikimaliza mafunzo yangu ya matibabu ya kisaikolojia, nilimchukua mgonjwa anayeitwa Tony. Alikuwa ameua watu watatu na kumkata kichwa mmoja wao.
Nilisoma ripoti nyingi za kutisha kuhusu wauaji wa kikatili lakini wakati huo kulikuwa na ushauri mdogo juu ya jinsi ya kuzungumza nao au kuwapa tiba, na kwa upande wangu nilijiuliza ikiwa kulikuwa na maana yoyote. Tutajuaje amekuwa "bora"?
Alikuwa na miaka 10 katika kifungo chake na hivi karibuni alikuwa amechomwa mswaki wenye ncha kali na wafungwa wengine watatu. Jaribio la kujiua lilikuwa limefuata.
Katika kikao chetu cha kwanza, kulikuwa na ukimya. Aliikunja mikono yake na kukwepa kukutana na macho yangu. Alipotazama juu, macho yake yalikuwa meusi sana yalionekana hivyo. Alikuwa akisumbuliwa na huzuni na ndoto mbaya. "Nilikuwa nikifikiria kuwa humu ndani kuna amani," alisema hatimaye, na kuvunja ukimya. "Kuna mtu kwenye chumba karibu na changu ambaye anaendelea kupiga kelele usiku."
Ilimchukua miezi kadhaa kufunguka kuhusu jinamizi lake la mara kwa mara. Ndani yake, alikuwa akimnyonga kijana mmoja ambaye alijigeuza kuwa baba yake. Ilituongoza kuzungumzia makosa yake na familia yake na jinsi, alivyokuwa mtoto, Tony aliteswa vibaya na baba yake; naye alianza kuwaonea wengine.
Baadaye nilifahamu kwamba mtu "katika chumba kilichofuata" ambaye alipiga kelele usiku alikuwa Tony mwenyewe. Nilipendekeza kwamba labda alikuwa akipiga kelele mambo ambayo hangeweza kueleza. Akainamisha uso wake mikononi mwake, akipunguza sauti yake. "Hapana ... sitaki," alikiri. "Siwezi kuwa dhaifu sana."
Nilifanya kazi na Tony kwa miezi 18 na nikaja kuhisi huruma na heshima kwa unyoofu wake, ingawa bado niliendelea kukumbuka maangamizi mabaya aliyosababisha. Ukweli kwamba aliomba tiba hii mwenyewe pia ilikuwa ishara kwamba kwa sehemu tayari alikuwa hatarini.
Watu waovu dhidi ya akili ovu
Linapokuja suala la wauaji wa kikatili kwa ujumla inachukuliwa kuwa wao ni watu wenye matatizo ya akili , lakini sikuwa na hakika kwamba inatumika kwa Tony.
Wataalamu wa magonjwa ya akili hawawezi kuomba msaada kwa vile hawataki kufanya jambo lolote ambalo wanaona kuwa la kudhalilisha, kwa hivyo kwa msingi huo tu Tony hangekidhi vigezo, kwani aliomba matibabu.
Saikolojia ambazo nimekutana nazo katika taaluma yangu hazijaweza kung'aa sana au za kijamii, au za kupendeza hata kidogo. Kwa kawaida hawana huruma kiasi kwamba hawawezi kuona matokeo waliyo nayo kwa wengine.
Na kinyume na imani iliyozoeleka, ni wauaji wachache sana ambao kwa kweli ni watu wenye matatizo ya akili, hasa wahalifu wa mauaji ya nyumbani kama vile wanandugu Menendez.

Chanzo cha picha, Getty Images
Hadithi ya Tony pia ilionesha kuwa shida za utotoni zinaweza kuwa sababu ya uhalifu. Ndugu hao wa Menendez walidai kuwa walikuwa waathiriwa wa unyanyasaji wa kimwili na kingono mikononi mwa baba yao, utetezi ambao ulipingwa mahakamani kabla ya kuhukumiwa kifungo cha maisha jela.
Bado idadi kubwa ya watu wamekumbwa na kiwewe kikali cha utotoni , kama asilimia 10-12 ya watu nchini Uingereza kulingana na tafiti nyingine,lakini idadi ndogo zaidi hufanya vitendo vya jinai vya unyanyasaji.
Swali ni nini hufanya watu wengine kujibu kiwewe cha utotoni kwa ukatili, wakati wengine hawajibu? Je, yawezekana kwamba watu hao ni "wahalifu"? Au, kama baadhi ya wagonjwa wangu walivyosema hapo awali: "Nimefanya mambo maovu, lakini je, hilo linanifanya kuwa mwovu?"
Hakuna ushahidi wa kisayansi kwamba watu wanazaliwa "waovu". Na katika uzoefu wangu, hakuna kitu kama mtu mbaya, badala yake, kuna hali mbaya za akili.
Kwa hivyo, kwa kawaida, naanza jibu langu kwa kuwaambia kwamba inawezekana kwa mtu yeyote kuingia katika hali hii ya akili, ambayo inaongozwa na hisia za kawaida za chuki, husuda, uchoyo na hasira.
Moyoni wengi wetu tuna uwezo wa ukatili lakini sababu za hatari zinazowafanya baadhi ya watu kutenda hivyo kwa unyanyasaji uliokithiri ni mahususi. Ni kidogo kama nambari kwenye kufuli ya baiskeli. Kama vile nambari zote zinavyopaswa kujipanga ili kufuli ya baiskeli kufunguka, sababu nyingi za hatari huwa zinakuwepo kabla ya vurugu kuzuka.
Sababu za hatari za kawaida ni kuwa kijana mdogo na wa kiume (mwenye viwango vya juu vya uchokozi); ulevi wa dawa za kulevya na pombe; kuwa na historia ya migogoro ya familia na kuvunjika kwa familia na historia ya uvunjaji wa sheria za kupambana na uhalifu.
Sababu muhimu zaidi ya hatari kwa mauaji, hata hivyo, ni asili ya uhusiano na mwathirika, hasa historia ya migogoro ya uhusiano. Inajulikana kuwa wanawake mara nyingi huuawa na wapenzi wa kiume au wanafamilia, na watoto wengi huuawa na wazazi wao au wazazi wa kambo. Mauaji ya watu wasiowajua ni nadra, na hizi huwa ni visa ambapo wahalifu huwa na hali mbaya ya afya ya akili.
Habari njema ni kwamba katika kipindi cha miaka 20 iliyopita kumekuwa na kushuka kwa viwango vya mauaji nchini Uingereza na kwingineko, ambayo kwa kiasi kikubwa ni matokeo ya mabadiliko katika baadhi ya vipengele tulivyovieleza awali.
"Kupungua kwa viwango vya mauaji tangu 2004 nchini Uingereza, ambayo pia yametokea Marekani, Hispania, Italia na Ujerumani, kunatokana na mabadiliko ya mtindo wa maisha kama vile kupunguzwa kwa unywaji pombe kupita kiasi na uvutaji wa bangi miongoni mwa vijana," anasema Profesa Manuel. Eisner, mkurugenzi wa Taasisi ya Criminology katika Chuo Kikuu cha Cambridge.
"[Pia] kwa kiasi fulani ni ushawishi wa teknolojia kama vile simu za mkononi na kamera za CCTV, ambazo huongeza ufuatiliaji na fursa za kupata usaidizi katika hali hatari."
Aidha, anahusisha kushuka kwa mabadiliko makubwa zaidi ikiwa ni pamoja na kuimarishwa kwa mila na desturi zinazopinga uonevu, na unyanyasaji dhidi ya wanawake, wasichana na watoto.
Na ingawa kuna watu wachache ambao akili zao haziwezi kubadilishwa, ambao watakuwa hatari kila wakati, kwa kuzingatia masimulizi yaliyopotoka katika visa vingi, tunaweza kutafuta njia za kubadilisha mawazo hayo mabaya kwa namna bora.
Imetafsiriwa na Lizzy Masinga na kuhaririwa na Ambia Hirsi












