Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi: Ni Liverpool pekee inaweza kumsajili Guehi - Crystal Palce

Chanzo cha picha, Getty Images
Klabu ya Crystal Palace inaamini ni Liverpool pekee ndio wanaweza kumsajili Marc Guehi, 25, mwezi Januari. Beki huyo wa England atakuwa mchezaji huru msimu ujao mkataba wake utakapokamilika. (Sky Sports)
Inter Milan na Manchester United zinajadiliana na wakala wa Karim Adeyemi, huku mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani, 23, akiwa tayari kuondoka Borussia Dortmund. (Bild - kwa Kijerumani)
Mshambuliaji wa Al-Ahli na timu ya taifa ya England, Ivan Toney yuko tayari kupunguziwa mshahara ili arejee katika Ligi ya EPL mwezi Januari, huku Tottenham na Everton wakimuwania mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29. (Team talk)
Beki wa Uholanzi Nathan Ake, 30, ni mmoja wa wachezaji watatu wa Manchester City wanaotathmini mustakabali wao kabla ya muda wa uhamisho wa wachezaji wa mwezi Januari kuwadia. ( Mail- usajili unahitajika)
Manchester United itaendelea kumfuatilia kiungo wa kati wa Real Madrid na Ufaransa Aurelien Tchouameni, 25, licha ya klabu hiyo ya Uhispania kukataa ofa ya thamani ya euro milioni 90 (£79.4m). (Fichajes - kwa Kihispania)
Napoli imempata mbadala Kobbie Mainoo, lakini mchezaji huyo wa Manchester United, 20, anasalia kuwa chaguo lao la kwanza. (La Gazzetta dello Sport via Football Italia)
Juventus imefanya mazungumzo ya awali kwa ajili ya mlinzi wa Lecce Tiago Gabriel, 20, huku Brentford pia wakimtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno chini ya miaka 21. (Tuttosport - kwa Kiitaliano)

Chanzo cha picha, Getty Images
Atletico Madrid wamekuwa wakimfuatilia beki wa kushoto wa Chelsea na Uhispania Marc Cucurella kwa miezi kadhaa, na wanafikiria kuwasilisha ofa ya thamani ya euro milioni 40 (£35.3m) kumsajili mchezaji huyo aliye na umri wa miaka 27. (Fichajes - kwa Kihispania)
Besiktas inapanga kumsajili mlinda lango wa Barcelona na Ujerumani Marc-Andre ter Stegen, 33, kwa mkopo, na kumpa mkataba wa kudumu akiridhia mpango huo. (Sport - kwa Kihispania)
Tottenham Hotspur iko mbioni kumsaka kipa wa "kiwango cha kimataifa" mwezi Januari. (Mail - usajili unahitajika)















