Vyakula maarufu zaidi wakati wa daku na kufunga katika nchi za Afrika

Muda wa kusoma: Dakika 2

Wakati wa mfungo wa mwezi wa Ramadhani, kuna ongezeko la hamu ya kula vyakula mbalimbali.

Wengine hufikiria manufaa ya afya na mazingira wanapochagua kile wanachokula kwa kiamsha-kiamsha kinywa au chakula cha kufungua .

Wakati familia zikitafakari asili ya mfungo wao wa Ramadhani na mlo wa kabla ya alfajiri, tulizungumza na baadhi ya wawakilishi wetu kutoka nchi za Afrika ili kujua ni vyakula gani huliwa sana katika nchi zao kwa ajili ya milo ya kabla ya alfajiri na mfungo wa Ramadhani.

Morocco

"Wakati wa kufuturu, tunaanza na tende na maziwa. Kisha tunakula kile tunachokiita harira - aina ya uji ambao ni kama supu na ni mtamu, unaotia nguvu na kupasha joto tumbo," anasema mwandishi wa BBC Basma El Atti.

Wakati wa sahur, "mara nyingi tunakula kitu kinachoitwa Sellou - kipande cha mkate na karanga, na kisha tunakunywa maji mengi."

Tanzania

Nchini Tanzania waumini hula Mihogo ya nazi, viazi vitamu, samaki, nyama na tambi. Mara nyengine hula magimbi, maharage na vitu vya ngano kama maandazi na chapati

Nigeria

Ahmed Ambali kutoka Nigeria anasema, "Wakati wa mfungo, tunapendelea kula chakula chepesi. Tunakula kwa nguvu na shauku nyingi. Chakula chepesi ni bora baada ya tumbo tupu kwa muda mrefu."

Vipi kuhusu sahur?

"Ni kweli kwamba tunameng'enya chakula wakati wa sahur - kama vile wanakula kwa ndimi zao."

Senegal

Watu wa Senegal "Wakati wa mfungo, tunakunywa chai ya mitishamba iliyo na viungo vya dawa na tende.

Huu ni mchanganyiko ambao utasaidia kusafisha tumbo," alisema Khadidiatou Cisse.

Aliongeza, "Kwa sahur, kila mtu hula vitu tofauti, haswa wali uliopikwa, lakini tunatumia supu ya mboga."

Kenya

"Tunakula samosa, bhajia na chapati kabla ya kula mlo mzito kama pilau," anasema Nasteha Mohammed.

Kwa suhur, "tunapendelea kula kitu chepesi kama chai, mtindi, chapati, na chakula chochote ambacho kinaweza kudumisha mwili wako kwa siku, hata wakati wa joto la mchana."