Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 28.09.2024

Muda wa kusoma: Dakika 3

Lille wako tayari kupokea ofa za Angel Gomes, Newcastle wanakabiliana na ushindani wa Marc Guehi na Manchester City wanapima uzito wa kumnunua Samuele Ricci.

Kiungo wa kati wa Uingereza Angel Gomes, 24, ndiye anayezungumziwa na vilabu vya Ligi ya Primia na Ulaya huku Lille wakijiandaa kupokea ofa za mchezaji huyo aliyepitia akademi ya Manchester United. (Telegraph – subscription required)

Newcastle United wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Liverpool na Manchester United ikiwa watawasilisha ombi lingine la kumsajili beki wa kati wa Uingereza Marc Guehi, 24, kutoka Crystal Palace mwezi Januari. (Football Insider).

Pia unaweza kusoma:

Manchester City wanafikiria kumnunua kiungo wa kati wa Torino na Italia Samuele Ricci, 23, kujaribu kuziba pengo la mchezaji wao wa kimataifa wa Uhispania Rodri, 28, anayeuguza jeraha. (Guardian)

Liverpool wanapanga kurekebisha safu yao ya ushambuliaji 2025 na wanatazamia kumnunua winga wa Borussia Dortmund ya Ujerumani Karim Adeyemi, 22. (Teamtalk)

Winga wa Uingereza Anthony Gordon, 23, anakaribia kusaini mkataba mpya wa miaka sita na Newcastle, ambao utakuwa pigo kwa wanaomwinda Liverpool. (Mirror)

Liverpool wanavutiwa na kiungo wa Freiburg Merlin Rohl, 22, ambaye ameiwakilisha Ujerumani katika timu ya under-21. (Bild)

Arsenal hawana nia ya kumuuza Takehiro Tomiyasu, 25, licha ya mlinzi huyo wa Japan kuhusishwa na kuhamia Inter Milan Januari. (Football Insider)

Barcelona wako tayari kumlipa mchezaji anayelengwa na Manchester United Frenkie de Jong mshahara wake ulioahirishwa - wa euro 18m (£15m) - kwa masharti kuwa kiungo huyo wa kati wa Uholanzi, 27, akubali kuondoka katika klabu hiyo msimu ujao wa joto. (FootballTransfers)

Manchester United na Manchester City zote zinamtaka mchezaji wa Bayer Leverkusen na Uholanzi Jeremie Frimpong, 23. (Football Insider)

Wolves wameambiwa watahitaji kulipa pauni milioni 40 ili kupata huduma ya winga wa Burnley na Italia wa timu ya under-21, Luca Koleosho, 20, ambaye pia anawindwa na Nottingham Forest na Newcastle. (Football Insider)

Manchester United imepokea kibali cha Ligi Kuu ya Uingereza kumsajili mshambuliaji wa Denmark Chido Obi-Martin,16, kutoka Arsenal. (Manchester Evening News)

Kiungo wa kati wa Arsenal wa Italia Jorginho, 32, anafikiria kuhamia katika nafasi ya ukocha na The Gunners mkataba wake wa sasa utakapokamilika 2025. (FootballTransfers)

Pia unaweza kusoma:

Imetafsiriwa na Asha Juma