Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 27.09.2024

Muda wa kusoma: Dakika 3

Marc Guehi amevutiwa na nia ya Liverpool kutaka huduma zake, Florian Wirtz halengwi na The Reds na Newcastle ipo katika mazungumzo ya kandarasi ya Anthony Gordon.

Mlinzi wa Crystal Palace na England Marc Guehi, 24, atachangamkia fursa yakujiunga na Liverpool na sio Newcastle ambao wamekuwa wakimezea mate kwa muda mrefu. (Football Insider)

Liverpool hawana nia ya kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Florian Wirtz, 21 kwa pauni milioni 100. (Echo).

Newcastle wanatatizika kuendeleza mazungumzo ya kandarasi na winga wao Muingereza Anthony Gordon, 23, ambaye alilengwa na Liverpool msimu uliopita wa joto. (Telegraph )

Chelsea walifanya mazungumzo kadhaa na AC Milan msimu wa joto kuhusu mlinda lango wa Ufaransa Mike Maignan, 29, lakini wakakatishwa tamaa na thamani iliyotolewa na timu hiyo ya Serie A ya euro 80m (£66.8m). (Corriere dello Sport, kupitia Metro)

Liverpool wangesaidia kufadhili mpango wa kumleta Gordon kwa kumuuza mlinzi wa Uingereza Joe Gomez, 27, kwa Newcastle kwa ada ya pauni milioni 45(Mirror),

Newcastle wanataka kumfunga Gordon kwa mkataba wa muda mrefu, huku Arsenal pia wakimtaka mchezaji huyo wa zamani wa Everton (Sun)

Chaguo la kwanza la Trent Alexander-Arnold atasaini mkataba mpya na Liverpool wakati beki huyo wa pembeni wa England mwenye umri wa miaka 25 atakapomaliza kandarasi yake msimu ujao wa joto. (Football Insider)

Muda wa Meneja Erik ten Hag huko Manchester United ni wa kuazima, kwani klabu hiyo inasawaka wagombeaji wa nafasi yake(Teamtalk)

Kocha wa zamani wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer "atakubali kwa haraka" ikiwa ataombwa kurejea Old Trafford kama meneja. (ESPN)

Real Madrid wanafuatilia hatua za Nico Paz huko Como na wanaweza kukiamsha kipengele cha kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye umri wa miaka 20 ikiwa ataendelea kuonyesha kiwango kizuri cha mchezo akiwa na timu hiyo ya Serie A. (AS - kwa Kihispania)

Sean Dyche ameelezea wazi nia yake ya kutaka kusalia kama meneja wa Everton baada ya klabu kununuliwa - na kuwaongoza katika uwanja wao mpya. (Telegraph - usajili unahitajika)

Imetafsiriwa na Yusuf Jumah