Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wachezaji wa kutazama katika Ligi ya Mabingwa - kutoka kwa nyota hadi vigogo wenye makali ya kipekee
- Author, Emlyn Begley
- Nafasi, BBC Sport journalist
- Muda wa kusoma: Dakika 7
Ligi ya Mabingwa itarejea wiki hii, na wakati huu utaweza kutazama mambo muhimu kote katika BBC.
Kuanzia saa 22:00 siku ya Jumatano ya wiki za mechi za Ligi ya Mabingwa, kutakuwa na vivutio vya mechi baada ya mechi vinavyopatikana kwenye BBC iPlayer na tovuti ya BBC Sport na programu, pamoja na kipindi maalum cha Champions League Match of the Day kwenye BBC One saa 22:40.
Ili kuamsha hisia za kila mtu, BBC Sport imechagua wachezaji 25 nje ya Ligi Kuu wa kutazama msimu huu, kuanzia walio wazi hadi vijana wenye vipaji.
Kylian Mbappe, 25 (Real Madrid/France)
Mshambulizi Mbappe anahitaji kufunga mara mbili pekee ili kuingia katika orodha ya wafungaji 10 bora wa Kombe la Ulaya msimu huu. Lakini bado hajanyanyua kombe hilo.
Uhamisho wake kutoka Paris St-Germain kwenda kwa mabingwa wa kila mwaka wa Uropa Real Madrid inamaanisha huu unaweza kuwa mwaka wake.
Jude Bellingham, 21 (Real Madrid/England)
Kiungo Bellingham alivuka matarajio yote msimu uliopita, akifunga mabao 23 katika michuano yote huku Real Madrid ikishinda Ligi ya Mabingwa na La Liga.
Mabao yalikauka kidogo ingawa baada ya Krismasi , kando na mabao mawili makubwa mchezo wake wa Euro 2024 kwa England ulikuwa wa kuridhisha.
Je, anaweza kupiga hatua katika Ligi ya Mabingwa msimu huu?
Lamine Yamal, 17 (Barcelona/Spain)
Ni kijana anayevutia zaidi ulimwenguni. Winga huyo alijipatia umaarufu mkubwa akiwa Barcelona msimu uliopita, na kuvunja rekodi kadhaa akiwa na umri wa miaka 16.
Lakini alikua jambo la kimataifa kwenye Euro 2024, na kusaidia Uhispania kubeba kombe.
Je, anaweza kuhaisha kishindo msimu huu? Tayari ana mabao matatu ya La Liga.
Dani Olmo, 26 (Barcelona/Spain)
Ni nyota mwingine wa Uropa wa Uhispania, kiungo mshambuliaji anacheza mpira wa juu katika klabu ya Uhispania kwa mara ya kwanza.
Mchezaji wa Barca aliyesajiliwa majira ya kiangazi kutoka Leipzig amefunga katika mechi zake tatu za kwanza katika klabu hiyo.
Harry Kane, 31 (Bayern Munich/England)
Mshambulizi Kane anaanza tena msako wake wa kila mwaka wa kombe la kwanza.
Msimu uliopita alifunga mabao 44 akiwa na Bayern lakini hawakushinda taji lolote kwa mara ya kwanza katika zaidi ya muongo mmoja.
Je, hilo linaweza kubadilika chini ya bosi wa zamani wa Burnley Vincent Kompany?
Michael Olise, 22 (Bayern Munich/France)
Ni Mchezaji mwingine wa London huko Bayern, ingawa Olise alicheza mechi yake ya kwanza ya Ufaransa katika mechi za Ligi ya Mataifa ya mwezi huu.
Winga huyo, aliyesajiliwa kwa kiasi kikubwa majira ya kiangazi kutoka Crystal Palace, atatarajia kufanya vyema katika msimu wake wa kwanza kucheza Ulaya.
Xavi Simons, 21 (Leipzig/Netherlands)
Kiungo huyo wa kati anayeweza kushambulia amerejea Leipzig kwa mkopo kutoka Paris St-Germain kwa msimu wa pili mfululizo.
Alifunga mabao 10 na kusajili asisti 15 katika mechi 43 msimu uliopita - na atajaribu kuboresha idadi hiyo wakati huu.
Antonio Nusa, 19 (Leipzig/Norway)
Nyota wa hivi punde wa Norway, winga Nusa alijiunga na Leipzig kutoka Club Bruges msimu huu wa joto - licha ya kulengwa na Chelsea, Tottenham na Brentford.
Tayari amefunga mara mbili kwa klabu yake mpya, ambayo inampeleka nusu ya msimu wake wa ufungaji bora tayari.
Julian Alvarez, 24 (Atletico Madrid/Argentina)
Mshambulizi Alvarez tayari amefunga mabao manane ya Ligi ya Mabingwa na kushinda kombe hilo - lakini huu utakuwa msimu wake wa kwanza kama mchezaji mkuu katika timu.
Atletico Madrid wanatarajia kumsajili baada ya kulipa pauni milioni 81.5 kumsajili kutoka Manchester City.
Conor Gallagher, 24 (Atletico Madrid/England)
Kiungo Gallagher hatimaye alikamilisha uhamisho wake kwenda Atletico Madrid kutoka Chelsea - na inaonekana ametulia vizuri.
Nguvu na uwezo wake unaweza kumfanya kuwa kipenzi cha bosi wa Atleti Diego Simeone.
Joao Neves, 19 (Paris St-Germain/Portugal)
Kiungo Neves alijiunga na PSG kutoka Benfica kwa ada ya takriban £50m, katika mojawapo ya usajili mkubwa zaidi wa majira ya joto.
Tayari ameshaichezea Benfica mechi 75 za kikosi cha kwanza, nne akiwa na PSG na kushinda mechi 11 akiwa na Ureno, licha ya kuwa bado ni kijana.
Desire Doue, 19 (Paris St-Germain/France)
Ni Kijana mwingine aliyegharimu pesa nyingi kujiunga na PSG msimu huu wa joto - walilipa pauni milioni 42 kumsajili kiungo mshambuliaji wa Rennes, Doue.
Tottenham na Bayern Munich pia walikuwa wamemtaka chipukizi huyo anayevutia, ambaye anaweza kucheza kama winga au nafasi ya kati.
Viktor Gyokeres, 26 (Sporting CP/Sweden)
Gyokeres anachukuliwa kuwa mmoja wa washambuliaji hatari zaidi barani Ulaya, licha ya kuwa bado hajacheza katika moja ya ligi kuu.
Amecheza katika daraja la pili nchini Uswidi, Ujerumani na Uingereza - kwa Swansea na Coventry - na amefunga mabao 51 katika michezo 56 ya Sporting.
Huu utakuwa msimu wake wa kwanza kwenye Ligi ya Mabingwa.
Ademola Lookman, 26 (Atalanta/Nigeria)
Winga Lookman amekuwa mtu mpya tangu ajiunge na Atalanta mwaka 2022, akifunga mabao 33 ndani ya miaka miwili tu - ikiwa ni pamoja na mabao matatu kwenye fainali ya Ligi ya Europa dhidi ya Bayer Leverkusen.
Mchezaji huyo mzaliwa wa London alishindwa kufikisha takwimu mbili katika msimu wake wowote nchini Uingereza na atakuwa na matumaini ya kuongeza dakika 61 za uzoefu wa Ligi ya Mabingwa aliokuwa nao Leipzig.
Angel Gomes, 24 (Lille/England)
Mchezaji mpya wa kimataifa wa England Gomes anasalia kuwa mchezaji mdogo zaidi wa Manchester United katika Ligi ya Premia, baada ya kucheza mechi yake ya kwanza akiwa na umri wa miaka 16 mwaka 2017.
Lakini ni huko Lille ambapo mchezaji huyo wa kiungo anayenyumbulika ametengeneza jina lake, na kutengeneza Ligue 1 ya juu kati ya asisti nane msimu uliopita.
Georgi Sudakov, 22 (Shakhtar Donetsk/Ukraine)
Kiungo huyo mahiri alikataa nafasi ya kuhamia Juventus na Napoli mapema mwaka huu na kusalia Shakhtar Donetsk, licha ya kuendelea kwa uvamizi wa Ukraine na Urusi.
Sudakov atakuwa akipania kampeni nyingine nzuri ya Ligi ya Mabingwa, baada ya kuzifumania nyavu dhidi ya Barcelona msimu uliopita.
Arne Engels, 21 (Celtic/Belgium)
Celtic wametumia pesa nyingi msimu huu wa joto kwa usajili wa rekodi ya kilabu ya pauni milioni 11 wa kiungo Engels, ambaye alicheza kwa mara ya kwanza Ubelgiji mapema mwezi huu.
Alikuwa mchezaji wa kawaida wa Augsburg katika Bundesliga msimu uliopita katika nafasi mbalimbali, zikiwemo eneo la kiungo na beki wa kulia.
Florian Wirtz, 21 (Bayer Leverkusen/Germany)
Florian Wirtz amekuwa uwanjani kwa miaka mingi lakini bado ana umri wa miaka 21 pekee. Amekuwa Bayer Leverkusen na, kwa ushindi wao wa mara mbili wa Ujerumani msimu uliopita, kelele za kumtaka asonge mbele ili kushinda mataji zinaweza kuisha.
Mabao 12 kati ya 44 aliyofunga Leverkusen yamepatikana kwenye Ligi ya Europa, lakini huu ni msimu wake wa kwanza katika mashindano makubwa ya Uropa.
Jeremie Frimpong, 23 (Bayer Leverkusen/Netherlands)
Frimpong alicheza vyema msimu uliopita kama beki wa pembeni wa kulia katika timu ya Leverkusen ya Xabi Alonso ambayo ilikuwa karibu kutozuilika.
Alifunga mabao 14 na kutoa pasi nyingine 12 katika mashindano yote. Je, anaweza kuchukua Ligi ya Mabingwa kwa kishindo?
Martin Baturina, 21 (Dinamo Zagreb/Croatia)
Kiungo huyo anayedaiwa kuwa Luka Modric ajaye, amekuwa akihusishwa na Juventus na Arsenal lakini bado yuko Dinamo Zagreb kwa sasa.
Sehemu ya kikosi cha Croatia Euro 2024, huu ni msimu wake wa pili katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa baada ya 2022-23.
Serhou Guirassy, 28 (Borussia Dortmund/Guinea)
Mshambulizi Guirassy alijiunga na Borussia Dortmund kwa pauni milioni 15 msimu huu wa joto, baada ya msimu mpya wa Stuttgart kumalizika akiwa amefunga mabao 28 katika michezo 28 ya Bundesliga - akiwa na umri wa miaka 28.
Alikuwa na bahati mbaya kutoshinda tuzo ya mfungaji wa mabao mengi, huku mpinzani wake wa Bundesliga, Kane, akiwa ndiye mchezaji pekee aliyefunga zaidi katika ligi tano bora za Ulaya.
Huu ni msimu wake wa pili katika Ligi ya Mabingwa baada ya kampeni ya 2020-21 akiwa na Rennes - alipofunga bao dhidi ya Chelsea.
Anatoliy Trubin, 23 (Benfica/Ukraine)
Kipa wa Ukraine Trubin anaingia msimu wake wa tano katika Ligi ya Mabingwa akiwa na Shakhtar Donetsk na Benfica - sio mbaya kwa mchezaji wa miaka 23.
Tayari ameshacheza mechi 37 barani Ulaya, ikijumuisha Ligi ya Europa na mechi za kufuzu.
Bobby Clark, 19 (Salzburg/England)
Kiungo wa kati wa England chini ya miaka 20 Clark alikuwa mmoja wa wanaoitwa watoto wa Jurgen Klopp katika Liverpool msimu uliopita, akicheza mara 12. Akawa mfungaji wao mdogo zaidi kuwahi kupachika mabao barani Ulaya kwa bao la Ligi ya Europa dhidi ya Sparta Prague.
Anatarajia kupata muda mwingi zaidi wa kucheza msimu huu baada ya uhamisho wa £10m kwenda Austria kuichezea Salzburg, inayosimamiwa na msaidizi wa zamani wa Liverpool Pep Lijnders.
Kenan Yildiz, 19 (Juventus/Turkey)
Mmoja wa vijana wenye vipaji vya kusisimua wa Uturuki kwenye Euro 2024, kiungo mshambuliaji Yildiz atatumai kucheza mechi yake ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa msimu huu.
Aliichezea Juventus mara 32 msimu uliopita, akifunga mabao manne.
Johan Bakayoko, 21 (PSV/Belgium)
Winga huyo wa Ubelgiji alifunga mabao 14 na kutoa pasi 14 za mabao kwa mabingwa wa Uholanzi PSV katika mashindano yote msimu uliopita.
Hakuna shaka kuhusu azma yake - anasema anataka kushindania tuzo ya Ballon d'Or ndani ya miaka mitano.
Imetafsiriwa na Yusuf Jumah na kuhaririwa na Seif Abdalla