Je, kahawa hubadilisha jinsi miili yetu inavyopokea virutubisho vya mwili?

Coffee being poured from a machine

Chanzo cha picha, Getty Images

    • Author, Giulia Granchi
    • Nafasi, BBC Brasil
  • Muda wa kusoma: Dakika 6

Ikiwa umewahi kuonywa kuwa usinywe kahawa wakati unapokula mlo wako, au mara kula mlo ni kwa wazo kuwa linaweza kuwa jambo baya kwa afya, ikawa kuna uweli kuhusu hili.

Kuna zaidi ya viungo 1000 vya kemikali katika kahawa, na vichache kama vile kafeini, polyphenols, na tannins, viinaweza kuingilia kati jinsi- mwili unavyopokea virutubisho kutoka kwa chakula chako.

Habari njema ni kwamba kwa watu wengi, athari hizi ni ndogo – na huenda kemikali hizi zisiwe nyingi vya vya kutosha kusababisha upungufu wa virutubisho vya mwili.

Virutubisho ni vitu vinavyopatikana katika chakula na vinywaji vyetu ambavyo hufanya kazi fulani muhimu katika mwili. Tunahitaji virutubisho tofauti ili kuwa na afya.

"Sio ufyonzwaji wote 'umezuiwa' kabisa - kunaweza kuwa na kupungua," anasema Alex Ruani, mtafiti wa udaktari wa Chuo Kikuu cha London katika elimu ya sayansi ya lishe na mwalimu mkuu wa sayansi katika Chuo cha Sayansi ya Afya.

Athari inategemea nguvu ya kahawa; kiasi cha virutubisho vinavyotumiwa, na sababu za hatari za mtu binafsi kama vile umri, kimetaboliki, hali ya afya na maumbile, Ruani anaelezea.

Virutubisho tunavyozungumzia ni pamoja na kalsiamu, chuma, na vitamini B.

Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi ikiwa "viwango vyako vya virutubishi tayari vinatosha, lakini kwa wale walio kwenye hatari ya upungufu au walio tayari na viwango vya chini vya virutubisho, unywaji wa kahawa kupita kiasi unaweza kuchangia kupungua zaidi," anasema Emily Ho, mkurugenzi wa Taasisi ya Linus Pauling na profesa katika Chuo cha Afya katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Oregon.

Pregnant woman in a waiting room with a notepad and pen

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wanawake wajawazito mara nyingi huwa katika idadi ya watu ambao wanahitaji kufuatilia viwango vyao vya madini ya chuma ambavyo vinaweza pia kuathiriwa na unywaji wao wa kahawa

Nani anapaswa kuwa muangalifu kuhusu kahawa anayokunywa?

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Tangu miaka ya 1980, tafiti zimehusisha kahawa na viwango vya chini vya madini ya chuma.

"Unapokunywa kahawa pamoja na chakula, polyphenols zilizopo ndani yake zinaweza kushikamana na madini fulani katika mfumo wako wa usagaji chakula," anasema Ho.

Anaeleza kuwa mchakato huu unaweza kufanya iwe vigumu kwa mwili wako kupokea madini ya chuma - kwani madini yanapaswa kupita kwenye seli za utumbo ili kuingia kwenye damu. "Ikiwa yatakwama kwenye polyphenols, hupita tu kwenye mwili wako na kutolewa."

Hii ni muhimu sana kwa madini ya chuma, hasa aina inayopatikana katika vyakula vinavyotokana na mimea, inayoitwa . Madini ya chuma yasiyo na heme( yanayotokana na vyakula kama vile matunda na mboga) ni vigumu kwa mwili kunyonya.

Polyphenols katika kahawa - hasa asidi ya klorojeni - inaweza kushikamana na aina hii ya chuma, kuizuia kufyonzwa ndani ya damu vizuri. Matokeo yake , chuma kinabaki kukwama kwenye utumbo wakati chakula kinaposonga kupitia mfumo wa mmeng'enyo wa chakula. Hatimaye hutolewa badala ya kutumiwa na mwili.

Yote haya inamaanisha kwamba watu walio na upungufu wa upungufu wa damu (anemia) wanapaswa kuwa waangalifu kuhusu kunywa kahawa karibu sana na milo yenye madini ya chuma.

"Inaweza kuwa bora kufurahia kahawa yako angalau saa moja kabla au saa chache baada ya kula vyakula vyenye madini ya chuma ili visichanganyike ndani ya tumbo lako," anasema Alex Ruani

Wanawake wanaopata hedhi na wajawazito mara nyingi huwa miongoni mwa watu ambao wanahitaji kuwa makini na viwango vyao vya madini ya chuma . Kwa kawaida wanahitaji chuma zaidi na wanakabiliwa na upungufu wa damu kwa hivyo wanapaswa kuwa makini na unywaji wao wa kahawa.

A man drinking from a paper coffee cup

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Uchunguzi unaonyesha kafeini inaweza kufanya iwe vigumu kwa mwili wako kushikilia kalsiamu

Madini ya kalsiam

Kalsiamu ni muhimu kwa afya ya mifupa, lakini 9% ya watoto wa miaka 16-49 nchini Uingereza hutumia chini ya Ulaji wa kiwango cha chini cha madini ya Kalsiamu (LRNI) kupitia chakula chao. Upungufu huu unawaweka katika hatari ya kuwa na mifupa dhaifu baadaye maishani.

Figo zetu huondoa taka na maji ya ziada kutoka kwa damu (kama mkojo) na kusaidia kuweka kemikali (kama vile sodiamu, potasiamu, na kalsiamu) sawa mwilini. Pia hutengeneza homoni.

Uchunguzi unaonyesha kafeini inaweza kufanya iwe vigumu kwa mwili wako kushikilia kalsiamu kwa kuingilia jinsi inavyojisindika kwenye figo zako na kufyonzwa ndani ya utumbo.

Tena, athari hizi ni ndogo na muhimu zaidi kwa watu ambao tayari wanakula lishe ya chini kiwango cha chini cha kalsiamu au wako katika hatari kubwa ya maswala ya afya yanayohusiana na mifupa.

"Utafiti maarufu uliochapishwa katika jarida, Osteoporosis International, unapendekeza kwamba kafeini inaweza kuchangia upotezaji wa mfupa kwa kuingilia utendaji wa mfupa," anasema Ruani. "Lakini tafiti zaidi zinahitajika ili kubaini athari halisi za kafeini kwenye hatari ya osteoporosis."

Kalsiamu inaweza kuhifadhiwa na mwili, kwa hivyo hauitaji kutumia kiasi kilichopendekezwa kila siku - lakini kwa kipindi cha miezi watu wazima wenye umri wa miaka 19-64 wanapaswa kuwa na wastani wa 700mg ya kalsiamu kwa siku.

Inafaa pia kuzingatia kwamba kafeini ina athari ya diuretic, i.e. kuongeza mara ngapi unahitaji kukojoa.

"Hii inaweza kusababisha upotezaji wa vitamini katika maji (kama vile vitamini B) na madini (kama vile chuma na kalsiamu), kwani utoaji una jukumu katika kudhibiti viwango vyake mwilini," anaongeza Ho.

Unaweza pia kusoma:

Vitamin B

"Kwasababu ya ushawishi wa kahawa kwenye utendaji wa figo na mtendaji wa virutubisho, kunywa kiasi kikubwa cha kahawa (kama vile vikombe vinne kwa siku au zaidi), kunaweza kusababisha kuongezeka la utoaji wa virutubisho mwilini kwa njia ya haja ndogo , na kwa hiyo, upotezaji wa vitamini kwa njia ya haja ndogo na kubwa , pamoja na vitamini B," anaelezea Ruani.

Vitamini B huyeyuka ndani ya maji, kwa hivyo hazihifadhiwa mwilini. Badala yake, ziada yoyote hutolewa kupitia mkojo.

Bowl of Kimchi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wataalam wa afya wanashauri kwamba vyakula vyenye probiotic, vyenye chachu , havipaswi kuliwa na kahawa

Probiotics

Probiotics ni bakteria hai na chachu wanaokuzwa kuwa na faida mbalimbali za kiafya.

Wanaweza kusaidia kurejesha usawa wa asili wa bakteria kwenye utumbo wako katika baadhi ya matukio, kulingana na tovuti ya NHS, lakini kuna ushahidi mdogo wa kuunga mkono madai mengi ya afya yaliyotolewa kuwahusu bakteria hawa.

Hata hivyo, ikiwa ungependa kujaribu virutubisho vya probiotic au vyakula vyenye probiotic kama vile mtindi na kimchi, ni bora kuepuka kuvitumia pamoja na vinywaji vya moto kama kahawa.

"Bakteria hai katika probiotics ni nyeti sana kwa joto, na kuathiriwa na joto la juu - kama vile joto katika kahawa - kunaweza kupunguza kiwango chao cha kuishi katika njia ya utumbo, na kuzifanya zisiwe na ufanisi," anasema Ruani.

Wakati mwingine huwekwa na madaktari ili kusaidia kupunguza kuhara kunakosababishwa na dawa za antibiotic, ili kupata faida ya juu subiri dakika 30-60 kabla ya kuchukua probiotic ikiwa umekunywa kikombe cha kahawa

Vintage image with cups of tea or coffee with a woman sipping a drink in the middle of the photo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Sio kahawa tu - vinywaji vingine vyenye kafeini nyingi vinaweza pia kuzuia ufyonzwaji wa virutubishi ikiwa utavinywa na milo

Je, inafaa kubadilisha unywaji wa kahawa kwa unywaji wa chai?

Iwapo unafikiria kunywa chai badala ya kahawa, ni muhimu kujua baadhi ya maswala sawa yanatumika kwa chai pia.

"Kwa kweli, polyphenols katika chai zinaweza kuwa na athari sawa juu ya upatikanaji wa virutubisho, kwa hivyo ni muhimu kuzingatia wakati wa unywaji wako wa chai ikiwa una wasiwasi juu ya ufyonzwaji wa virutubisho," anaonya Ho.

Unaweza pia kusoma:

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi