Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Vita vya Ukraine: Marekani yaidhinisha msaada wa $2.6bn kwa Ukraine na washirika
Marekani imeidhinisha karibu $2.7bn (£2.3bn) kama msaada mpya kwa Ukraine na washirika wake, ikiwa ni pamoja na $675m katika silaha za Ukraine inapopambana na Urusi.
Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin alitangaza fungu hilo lkwa ajili la silaha katika mkutano na mawaziri wenzake katika kambi ya anga ya Marekani huko Ramstein, Ujerumani.
Msaada huo ni pamoja na silaha za howitzers, silaha za kijeshi, magari ya Humvee, ambulensi za kivita na mifumo ya kuzuia mizinga.
Marekani tayari imeahidi angalau $13bn katika msaada wa kijeshi kwa Ukraine. Utawala wa Biden ulisema Alhamisi ulitenga $2bn katika usaidizi wa muda mrefu katika mfumo wa uwekezaji ili kuimarisha usalama wa Ukraine na majirani zake 18, wakiwemo wanachama wa Nato na wasio wanachama walio katika hatari ya uvamizi wa Urusi siku zijazo.
Ilisema itaarifu Congress juu ya mpango wa msaada.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken aliwasili katika mji mkuu wa Ukraine wa Kyiv, huku mwenzake akiwataka washirika wa Ukraine kujitolea kuisaidia nchi hiyo kwa muda mrefu kadri inavyohitajika na kuwa tayari kukabiliana na aina ya usaidizi unaotolewa.
"Inamaanisha kusonga mbele kwa haraka ili kuvumbua na kusukuma msingi wetu wote wa kiviwanda wa ulinzi ili kuipa Ukraine zana ambayo itazihitaji," Bw Austin alisema.
Akielezea uvamizi wa Urusi kama "vita haramu, vya kifalme visivyoweza kutetewa", alisema: "Sasa tunaona mafanikio yanayoweza kuonekana ya juhudi zetu za pamoja kwenye uwanja wa vita."
Siku ya Jumatano, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema hivi karibuni jeshi la nchi yake lilifanya mashambulizi yenye mafanikio dhidi ya vikosi vya Urusi vinavyodhibiti maeneo makubwa ya Ukraine kusini na mashariki na kutwaa tena makaazi karibu na mji wa kaskazini-mashariki wa Kharkiv.
Hakutoa maelezo lakini maafisa wote wa Ukraine na wanaoiunga mkono Urusi wanaripoti mapigano karibu na Balakleya, kilomita 60 (maili 38) kusini-mashariki mwa Kharkiv.
Waziri wa Ulinzi wa Uingereza Ben Wallace anasema kuna dalili kwamba Ukraine inapiga hatua kubwa kijeshi. Mizinga na roketi za masafa marefu zinazotolewa na nchi za Magharibi zinasaidia kulenga vituo vya usambazaji wa Urusi na vituo vya kutoa amri.
Rais wa Urusi Vladimir Putin alikanusha kurudishwa nyuma kwa mashambulizi siku ya Jumatano, akisema: "Hatujapoteza chochote na hatutapoteza chochote."
Urusi inasema inapambana na Wanazi mamboleo nchini Ukraine madai ambayo yamekanushwa na wengi na kwamba inatishiwa na uhusiano wenye nguvu wa muungano wa Nato na Ukraine.
Tangu uvamizi huo wa tarehe 24 Februari, Umoja wa Mataifa umerekodi vifo vya raia 5,718, huku 8,199 wakijeruhiwa, na zaidi ya Waukraine milioni saba wamerekodiwa kama wakimbizi kote Ulaya. Idadi isiyojulikana ya wapiganaji wameuawa au kujeruhiwa.
Urusi, ambayo ni msambazaji wa nishati duniani, imefungwa katika vikwazo vya kiuchumi na nchi za Magharibi ambayo iliweka vikwazo vikubwa katika kukabiliana na uvamizi huo.