Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Fahamu mifumo ya ulinzi ambayo Iran imetuma kwenda Urusi
Taarifa iliyotolewa wiki iliyopita kuhusu jeshi la Iran kupeleka droni Urusi haikuja kama jambo la kushangaza -taarifa kuhusu mipango ya Moscow ya kupata ndege zisizo na rubani (UAVs) kutoka kwa Tehran zilichapishwa mapema mwezi Julai, kulingana na uchambuzi wa mwandishi wa BBC Pavel Aksyonov.
Gazeti la Marekani Washington Post liliandika katika majaribio ya kwanza ya droni ambazo Urusi ilikuwa tayari imezipata kutoka kwa Iran.
Jeshi la Urusi lina zaa nyingi za kijeshi ambazo kwa sasa hazifanyi kazi. Hatahibyo taarifa kuhusu ni zana zipi hazitolewi.
Ingawa mpango wa ndege zisizokuwa na rubani za Iran umekuwa ukiandaliwa tangu mwishoni mwa mwa miaka ya 1980, nchi inakabiliwa na vikwazo, na wataalamu wanasema droni nyingi za Iran zimetengenezwa kwa kunakili miundo ya droni za kigeni.
Ikikabiliwa na ukosefu wa droni wakati wa vita vya Ukraine, Urusi ililazimika kuelekea Iran kwasababu kulikuwa na fursa chache za kununua aina hizo za silaha kutoka nchi nyingine na uzalishaji wa ndani ulikuwa wa kiwango cha chini, uchambuzi ulisema.
Droni za Iran
Licha ya masharti ya kupata teknolojia ya kigeni, Iran inafahamika kama mtenezaji wa droni. Nchi hii imekuwa chini ya vikwazo vya kimataifa kwa na imepitia uzoefu wa kuishi katika hali ngumu.
"Iran imekuw aikitengeneza ndege zisizokuwa na rubani tangu miaka ya 80 na imekuwa ikizipatia umuhimu. Ndio maana ina aina mbali mbali za droni, zikiwe mo za kimkakati, za utambuzi wa maeneo yanayolengwa na droni za mashambulio.
Iran ililazimika kuishi chini ya vikwazo na kununua kila kitu inachohitaji kuimarisha sekta yake ya jeshi licha ya vikwazo vinavyoikabili.
Nchini Iran, hazitengenezwi tu UAVs, makombora ya masafa marefu ya ballistic na silaha nyingine kali kama vile mradi wa nyuklia ambao unaendelea licha ya vikwazo vyote dhidi yake ,"mtaalamu wa kijeshi wa Israeli David Gendelman aliiambia BBC.
Iran haiwezi kubuni ndege ya kijeshi peke yake, lakini imejifunza kutathmini na kuiga kutengeneza nakala ya teknolojia ya kigeni wakati wa kipindi cha vikwazo, anasema mtaalamu.
Kwa njia hiyo, Wairan walijifunza ubunifu wa ndege ya kijesi ya Marekani- American Northrop F-5 na hata wakaweza kuanzisha ndege zo wenyewe.
Sekta ya Iran ina uzoefu mkubwa katika utengenezaji wa vipuli kwa ajili ya ndege za kijeshi, iliyorithi kutoka enzi ya Shah . Zaidi ya hayo, inaaminiwa kuwa Iran ilikwepa vikwazo na kununua vipuli mbalimbali na vitu vingine kutoka ng’ambo.
Urusi itanunua droni zipi ?
Kulingana kituo cha utafiti cha ndege zisizokuwa na rubani za kijeshi cha chuo cha Bard ,kufikia mwaka 2019, Iran daraja la 1, 2 na 3 la ndege hizo 179.
Daraja la kwanza lilijumuisha droni za kimkakati, quadcopters na aircraft, na daraja la pili na la tatu lilijumuisha droni za uzani wa kati na nzito ( UAVs ) ambazo zimewekwa katika kitengo cha "masafa marefu" kulingana na kimo chake (MALE UAV na HALE UAV).
Droni aina ya "Mohajer-6" iliyotolewa kwa Urusi iko katika daraja la pili kulingana na uainishaji huu . Kulingana na taasisi ya Globalsecurity.Org, Irani ilizitumia katika nchi ya Afghanstan miaka ya 1990.
Licha ya jina lake linalofahamika sana, "Shahed-129" na "Shahed-191" ndege hizi zisizokuwa na rubani ni tofauti na UAVs. Labda ni kwasababu zile za Magharibi zinazofanana nazozilikuwa tofauti pia.
Inaaminiwa kwamba "Shahed-129" zilibuniwa kwa misinhi ya droni za Israeli aina ya Hermes 450 ambazo ziliangukia mikononi mwa wahandishi wa Iran . "Shahed-191" ilitengenezwa kwa msingi wa droni za Marekani zinazofahamika kama American Q-170 Sentinel.
Shirika lisilo la kiserikali la Marekani la kupambana na nyuklia nchini Iran"United Against Nuclear Iran - UANI" katika ripoti yake "Tisho la mpango wa droni wa Iran " inasema kuwa inatumia droni za Mohajer na Shahed-129 katika nchi za Iraq na Syria. Ilisema kuwa droni hizi hushambulia maeneo yaliyolenhwa ndani ya Syria.
Iwapo Urusi ina nia ya katika UAVs za Iran, sio "kwasababu droni zao ni bora duniani," kwasababu utengenezaji katika Urusi yenyewe ni ni wa kiwango cha chini sana, yote kwa ubora na uwingi, anasema David Gendelman.
Kampuni ya Kronstadt nchini Urusi hutengeneza droni za Orion za aina ya MALE. Mwezi Disemba 2021, iliripotiwa kwamba droni hizi hata zilishambulia maeneo ndani ya Syria. Droni hizi za UAVs zinatengenezwa katika kiwanda cha Dubna, karibu na Moscow.
Mpango wa Iran ulitengeneza droni za UAVs kuanzia mwaka 1988, kulingana na uchagnanuzi wa BBC.