Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 01.09.2022

Chanzo cha picha, Getty Images
Chelsea wamepewa nafasi ya kumsajili Neymar, 30, wakati Paris St-Germain wakijaribu kumuuza mshambuliaji huyo wa Brazil ili kuepuka kukiuka miongozo ya Uefa ya usawa wa matumizi ya fedha (Mail)
Lakini wakati Chelsea wana nia ya kutaka kumnunua Neymar, kwa upande mwingine, Paris St-Germain sasa wanakataa kumuuza. (Times via Metro)
Mshambulizi wa AC Milan Rafael Leao, 23, na kiungo wa kati wa Dinamo Moscow Arsen Zakharyan, 19, wamehusishwa na Chelsea katika uwezekano wa kufanya uhamisho wa mara mbili. Zakharyan wa Russia angegharimu pauni milioni 12.6 lakini bei inayoripotiwa kuwa ya pauni milioni 126 inaweza kughairi uhamisho wowote wa Leao wa Ureno. (Times - requires subscription)

Chanzo cha picha, Getty Images
Beki wa pembeni wa Barcelona Sergiño Dest atajiunga na AC Milan kwa mkopo wa msimu mzima, na chaguo la kubadilisha uhamisho huo kuwa uhamisho wa kudumu wa €20m. Beki huyo wa Marekani alikuwa akihusishwa na kuhamia Manchester United(Fabrizio Romano)
Brentford wanatumai kuteka nyara uhamisho wa Arsenal wa kumnunua Mykhaylo Mudryk, 21, wa Shakhtar Donetsk, lakini itabidi kuvunja rekodi ya uhamisho ya klabu hiyo ili kumsajili mshambuliaji huyo wa Ukraine mwenye thamani ya pauni milioni 25. (Mirror)
Arsenal wamewasilisha ofa ya pauni milioni 20 kwa kiungo wa Palmeiras Danilo, 21, lakini klabu hiyo inataka ada ya juu zaidi kwa Mbrazil huyo. (Goal Brazil via Metro)
PSV Eindhoven wamekubali mkataba wa £34m kwa Gakpo huku Southampton ikijiandaa kuvunja rekodi ya uhamisho ya klabu hiyo. (Times - requires subscription)

Chanzo cha picha, Getty Images
Fenerbahce wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kumnunua fowadi wa Paris St-Germain Mauro Icardi, 29, huku mshambuliaji huyo wa Argentina tayari akiwindwa na timu ya Uturuki Galatasaray. (L'Equipe - in French)
The Blues wameweka dau la pauni milioni 43 kwa Alvarez huku Chelsea wakilenga kusajili mshambuliaji na kiungo kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Sky Sports)
Newcastle United wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili kiungo wa kati wa Leicester City na Ubelgiji Youri Tielemans, 25(Mail)
Arsenal imekuwa ikifuatilia Tielemans katika kipindi chote cha dirisha la usajili, lakini "klabu nyingine isiyojulikana" sasa iko tayari kuwasilisha ombi huku Leicester ikiweka bei ya pauni milioni 30. (Express)
Kiungo wa kati wa Ajax Edson Alvarez, 24, ana nia ya kutaka kuhamia Chelsea huku mmiliki Todd Boehly akizindua dau la pauni milioni 50 kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Mexico. . (De Telegraaf via Metro)

Chanzo cha picha, Getty Images
Barcelona wamekataa ofa ya mchezaji pamoja na pesa kutoka kwa Chelsea kwa mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 33. Wanataka €15m (£13m) pamoja na beki wa pembeni wa Uhispania Marcos Alonso, 31, lakini mazungumzo yanaendelea. (Fabrizio Romano)
Chelsea wanakaribia kufikia makubaliano ya pauni milioni 77.7 kumsaini beki wa Croatia Josko Gvardiol, 20, lakini watakuwa tayari kumruhusu abaki RB Leipzig kwa mkopo kwa msimu wa 2022-23. (Telegraph - requires subscription)
Leeds United inajiandaa kuwasilisha ofa kwa mlinzi wa Sheffield United ya Jamhuri ya Ireland John Egan, 29, lakini wanakabiliwa na hatari ya kumpoteza winga wa Wales Dan James, 24, kwa Tottenham(Express)
Southampton wako tayari kuongeza ofa yao kwa winga wa Uholanzi Cody Gakpo, 23, baada ya PSV Eindhoven kukataa ofa ya awali ya pauni milioni 21.4. (Telegraph - requires subscription)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambulizi wa zamani wa Everton James Rodriguez, 31, ana nia ya kuchezea klabu ya La Liga Sevilla - kwa sasa raia huyo wa Colombia yuko katika klabu ya Qatar Al-Rayyan. (El Chiringuito)
Beki wa Paris St-Germain na Senegal Abdou Diallo, 26, ambaye anahusishwa na kuhamia Aston Villa, atasafiri kuelekea Ujerumani siku ya Alhamisi kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu kabla ya kuhamia RB Leipzig. (Fabrizio Romano)
Birmingham City wapo kwenye mazungumzo na Manchester United katika jitihada za kumsajili kiungo wa kati wa Uholanzi Tahith Chong, 22, kwa mkataba wa kudumu. (Star)
Mshambuliaji wa Denmark na Nice Kasper Dolberg, 24, yuko Uhispania kukamilisha uhamisho wa mkopo kwenda Sevilla. (AS - in Spanish)












