Kujiuzulu kwa Boris Johnson: Kipi kinafanyika sasa?

PA Media

Chanzo cha picha, PA Media

Maelezo ya picha, Boris Johnson

Boris Johnson anatarajiwa kujiuzulu kama kiongozi wa chama cha Conservative na atajiuzulu kama Waziri mkuu punde tu kiongozi mpya atakapopatikana.

Atajiuzulu baada ya kuhudumu chini ya miaka mitatu katika wadhfa huo, licha ya kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa 2019. Mawaziri wakuu wanaoondoka afisini wanatarajiwa kisalia afisini hadi mrithi akapopatikana.

Je hilo linafanyiki vipi?

Kwanza chama hicho cha Conservative ni sharti kimpate kiongozi mpya.

Je Chama cha Conservative humchagua vipi kiongozi mpya?

Mara baada ya kiongozi wa Conservative kujiuzulu, uchaguzi wa kiongozi mpya wa chama unaanzishwa. Chini ya sheria za sasa, wagombea wanahitaji kuungwa mkono na wabunge wanane wa chama hicho ili kuwania.

Mara tu baada ya wagombea wote kuidhinishwa na iwapo ni zaidi ya wagombea wawili , wabunge wa chama hicho watashiriki katika uchaguzi hadi wagombea wawili watakaposalia.

Katika raundi ya kwanza , mgombea ni sharti ajipatie asilimia 5 ya kura ili kusalia katika kinyanganyiro.

Katika raundi ya pili ni sharti wajipatie asilimia 10 ya kura .

Katika raundi itakayofuata mgombea mwenye kura kidogo ataondolewa.

Wakati wabunge wawili watakaposalia , wanachama wote wa chama cha Conservative nchini - na sio wabunge watampigia kura mshindi.

 Muda wa uchaguzi huo huamuliwa na kamati ya kamati ya wabunge wa nyuma , na kamati hiyo itapiga kura kubadilisha sheria kabla ya uchaguzi huo kufanyika.

Je kiongozi mpya wa chama cha Conservative anachaguliwa vipi?

Uongozi wa Uingereza

Je Waziri mkuu mpya huchaguliwa vipi?

Yeyote atakayeibuka mshindi kuongoza chama cha Coservative , atakuwa kiongozi wa chama hicho chenye wabunge wengi.

Malkia atawataka kuunda serikali.

Je kutakuwa na uchaguzi mkuu?

Sio lazima.

Wakati Waziri mkuu anapojiuzulu sio lazima kufanyike kwa uchaguzi mkuu wa moja kwa moja.

Siku ya mwisho ambayo uchaguzi unaweza kufanyika ni Januari 2025, lakini Waziri mkuu mpya anaweza kuitisha uchaguzi kabla ya wakati huo.

Je Boris Johnson atasalia uongozini kwa muda gani?

Bwana Johnson ataendelea kuwa Waziri mkuu hadi mwisho wa msimu wa vuli , mwanndishi wa BBC Chris Mason ameripoti.

Hii ni kawaida kabisa. Atasalia madarakani hadi chama cha Conservative kitakapomchagua kiongozi mpya, kama watangulizi wake Theresa May na David Cameron walivyofanya walipojiuzulu.

Kwa nadharia, ikiwa angetaka kuondoka mara moja, Malkia angeweza kumteua kaimu kiongozi, pengine mjumbe wa Baraza la Mawaziri, kuchukua hatamu hadi kiongozi mpya apatikane.

Hiyo itakuwa hali isio ya kawaida.

Je ni nani anayeweza kumrithi Boris Johnson kama Waziri mkuu?

Je ni nani anayeweza kumrithi Boris Johnson kama Waziri mkuu?

Kwasasa hakuna mrithi wa moja kwa moja wa bwana Johnson , lakini kuna wagombea kadhaa.

Waziri wa zamani Jeremy Hunt na Sajid Javid wote wawili wamewania uongozi wa chama hicho na huenda wakawania tena.

Wagombea wengine:

Aliyekuwa Waziri Michael Gove

Waziri wa wa biashara ya Kimataifa Penny Mordaunt

Aliyekuwa Chansela Rishi Sunak

Waziri wa masuala ya kigeni Mwenyekiti wa kamati ya masula ya kigeni Tom Tugendhat,

Wazir wa ulinzi Ben Wallace

Chansela Nadhim Zahawi

Je Boris Johnson ana uwezo gani?

Hadi atakapoacha rasmi wadhifa wa Waziri Mkuu, Bw Johnson bado ana mamlaka yale yale, kinadharia. Ijapokuwa hana mamlaka ya kuanzisha sera zozote mpya.

Bado ataiwakilisha Uingereza nje ya nchi na anaweza kuendelea kufanya uteuzi wa umma au mabadiliko kwa timu yake ya mawaziri.

Mojawapo ya vitendo vyake vya mwisho ofisini huenda ikawa ni kutunuku ushujaa na kuteuliwa kwa Mawaziri bungeni.